Boda boda na Third Party Insurance

Boda boda na Third Party Insurance

Ti Go

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2012
Posts
985
Reaction score
1,004
Ni kwa uhakika uliowazi kuwa kwa sasa Bodaboda waliowengi wanatembeza piki piki zao kinyume na sheria za usalama barabarani. Wengi wao hawana leseni Na mbaya zaidi hawana hata third party insurance. Kwa mtazamo wa juu juu nafikiri huu ndio usafari unaotumiwa Na wasafiri wengi, iwe mijini au vijijini.

Kwa hiyo niseme ni hatari na ni kuweka rehani maisha ya wasafiri wanaotumia usafari huu kwa kutumia madreva wasio na ujuzi (leseni). Hawajadhibitishwa Na mamlaka za utoaji Wa leseni za vyombo vya usafiri. Kijana akishajua kuwasha piki piki basi anaingia barabarani kubeba abiri.

Mbaya ya yote piki piki haijakatiwa bima ya third party insurance. Maana yake hata akipata ajari, yeye pamoja Na abiria wake hawa kinga ya bima. Hakuna compensation yoyote.

Huko nyuma siasa ziliingilia kati, wanasiasa kwa sababu ya kutafuta wapiga kura wakazuia polisi Wa traffic kusimamisha hawa vijana. Hivyo wako huru barabarani, bila leseni, bila bima, wanakimbia bila kujali speed limit, wanabeba misikaki.

Hii ni hatari kwa abiria, ni hatari vijana hawa, hata Ni hatari kwa watembea kwa miguu kugongwa bila malipo! We need to do something!
Najua humu kuna wasomaji ambao Ni waendesha Boda Boda, wayapinga. Lakini ukweli ndio ulivyo.

Tujadiri kwa faida yetu sote.
 
Moderator naomba uhamishie hii mada kwenye jukwaa la habari na hoja mchanganyiko. Sikuwa Na lengo la kuiweka jukwaa la elimu
 
Mimi nazn Cha kwanz Ni Hao bima kusimamiw ili walipwe wanaopat madhar hak zao

Pk PK zingne znabima lkn sijaona Bima wakjlpa watu wa boda Boda
 
Back
Top Bottom