Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 893
- 1,021
BODABODA
Leo mie boda boda,
Nakikalia kigoda,
Upepo ni yangu poda.
Naipenda sana kazi,
Ndo inipayo malazi,
Kula mpaka mavazi.
Sina elimu kichwani,
Nina peni mkononi,
Na mawazo akilini.
Sinayo mapumziko,
Machweo na pambazuko,
Kila siku ni msako.
Safari zisoukomo,
Na siwezi fanya mgomo,
Si fungi wangu mdomo.
Kipo mbele kifo changu,
Uharaka ndo kula yangu,
Naujali muda wangu.
Na ni wa mwisho kulala,
Kutoka kabla ya sala,
Hii ndo yangu amala.
Ipi heshima stahiki,
Watuona mamluki,
Watu tuliojawa dhiki.
Sina leseni kazini,
Sinayo pesa ndani,
Naipataje leseni.
Polisi wetu adui,
Twakimbizana ja kui,
Urafiki haukui.
Sheria haiko kwetu,
Ja tuko kivyetu vyetu,
Nasi tuwe fungu letu.
Boda ni ya kuikodi,
Kaya nagongewa hodi,
Hapo nadaiwa kodi.
Vipi kuhusu ajali,
Nani atayenijali,
Ingali sina salali.
Similiki madolali,
Zaidi ya wangu usuli,
Na kalamu ya penseli.
[emoji3578]Abuuabdillah
0744883353
0718569091
Leo mie boda boda,
Nakikalia kigoda,
Upepo ni yangu poda.
Naipenda sana kazi,
Ndo inipayo malazi,
Kula mpaka mavazi.
Sina elimu kichwani,
Nina peni mkononi,
Na mawazo akilini.
Sinayo mapumziko,
Machweo na pambazuko,
Kila siku ni msako.
Safari zisoukomo,
Na siwezi fanya mgomo,
Si fungi wangu mdomo.
Kipo mbele kifo changu,
Uharaka ndo kula yangu,
Naujali muda wangu.
Na ni wa mwisho kulala,
Kutoka kabla ya sala,
Hii ndo yangu amala.
Ipi heshima stahiki,
Watuona mamluki,
Watu tuliojawa dhiki.
Sina leseni kazini,
Sinayo pesa ndani,
Naipataje leseni.
Polisi wetu adui,
Twakimbizana ja kui,
Urafiki haukui.
Sheria haiko kwetu,
Ja tuko kivyetu vyetu,
Nasi tuwe fungu letu.
Boda ni ya kuikodi,
Kaya nagongewa hodi,
Hapo nadaiwa kodi.
Vipi kuhusu ajali,
Nani atayenijali,
Ingali sina salali.
Similiki madolali,
Zaidi ya wangu usuli,
Na kalamu ya penseli.
[emoji3578]Abuuabdillah
0744883353
0718569091