Bodaboda, Bajaji, Daladala, Taxi sasa marufuku.

Bodaboda, Bajaji, Daladala, Taxi sasa marufuku.

Kwameh

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2011
Posts
1,793
Reaction score
2,152
RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2013

IBARA YA 25 ( 2 )

"Biashara ya kusafirisha binadamu ni marufuku katika Jamhuri ya Muungano."

Dukuduku langu: Wamiliki wa vyombo vya usafiri wa umma wanaotegemea sekta hii adhimu na
wananchi tusio na vyombo binafsi vya usafiri tutaishije katika enzi za Katiba mpya?
 
ha ha ha ha JF kweli kiboko. sio kwamba wanamaanisha ile ya kubeba wasomali?
 
Duh! ... Kwameh ... Pole ... wewe ndio umepotea kabisa.

Siyo masuala ya kusafirisha binadamu ni BIASHARA YA BINADAMU ... Yaani Human Trafficking.

What is Human Trafficking?

Human trafficking is a form of modern-day slavery where people profit from the control and exploitation of others.

Victims of human trafficking include children involved in the sex trade, adults age 18 or over who are coerced or deceived into commercial sex acts, and anyone forced into different forms of "labor or services," such as domestic workers held in a home, or farm-workers forced to labor against their will. The factors that each of these situations have in common are elements of force, fraud, or coercion that are used to control people. Then, that control is tied to inducing someone into commercial sex acts, or labor or services. Numerous people in the field have summed up the concept of human trafficking as "compelled service."

Article 3, paragraph (a) of the Protocol to Prevent, Suppress and Punish Trafficking in Persons defines Trafficking in Persons as the recruitment, transportation, transfer, harbouring or receipt of persons, by means of the threat or use of force or other forms of coercion, of abduction, of fraud, of deception, of the abuse of power or of a position of vulnerability or of the giving or receiving of payments or benefits to achieve the consent of a person having control over another person, for the purpose of exploitation. Exploitation shall include, at a minimum, the exploitation of the prostitution of others or other forms of sexual exploitation, forced labour or services, slavery or practices similar to slavery, servitude or the removal of organs
.

Last edited by a moderator:
Human-trafficking1.jpg
 
RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2013

IBARA YA 25 ( 2 )

"Biashara ya kusafirisha binadamu ni marufuku katika Jamhuri ya Muungano."

Dukuduku langu: Wamiliki wa vyombo vya usafiri wa umma wanaotegemea sekta hii adhimu na
wananchi tusio na vyombo binafsi vya usafiri tutaishije katika enzi za Katiba mpya?

Acheni upotoshaji....hawamaanishi usafiri wa taxi na daladala but human trafficking
 
acha kupotosha, unajua maana halisi halafu unakuja hapa makusudi kupotosha umma. Warioba team wanamaaanisha HUMAN TRAFFICKING
 
Hakusoma vizuri yupo kwenye viroba akisubiri foleni isogee
 
ha ha ha ha

ha ha ha ha hah....
Kaka zangu, mbona mnaicheka Katiba yetu mpya? Nadhani si nidhamu nzuri kuicheka rasimu adhimu iliyoandikwa na weledi wa Taifa letu.

Siyo masuala ya kusafirisha binadamu
Sio masuala ya kusafirisha binadamu?

Utasemaje sio masuala ya kusafirisha binadamua wakati wao wenyewe wamesema "Biashara ya kusafirisha binadamua ni marufuku katika Jamhuri ya Muungano."??

Hakusoma vizuri yupo kwenye viroba akisubiri foleni isogee
Niko kwenye viroba na sikusoma vizuri?

Inawezekana aliyeandika katiba anajua kwamba anawaandia watu wenye upembuzi wa ki-viroba viroba, ambao hawana umakini wa kuyapa uzito masuala ya kisheria na kikatiba, unaweza ukawaandikia kitu chochote cha kilevi levi halafu anaeona tatizo ndio anaambiwa amekunywa viroba. Zingatia hilo.

wanamaaanisha HUMAN TRAFFICKING
WEWE ndio unatafsiri hivyo. MIMI niruhusiwe pia haki ya kutafsiri na kujadili kwa mujibu wa yaliyoandikwa. WAO wamesema: "Biashara ya kusafirisha binadamu ni marufuku katika Jamhuri ya Muungano."

Kwa hiyo Bodaboda, Bajaji, Daladala, Taxi, Pantoni za vivukoni, Gari Moshi, Ngalawa za kulipia, sasa marufuku.
 
Ukingwendu, Tungo tata au kiswahili hakijitoshelezi kimsamiati? Chagua jibu sahihi/
 
The guy has a point Kwameh, kama rasimu ya katiba ilimaanisha 'human traficking' wangesema 'biashara ya ulanguzi wa binadamu' na ku-define neno 'ulanguzi' . Otherwise kwameh is right
 
Last edited by a moderator:
wazee wa 'wapigwe tu' wanaweza kuchukua hiki kipengele na kukitumia kama mleta thread alivyoelezea.wataalamu wa kiswahili watupe neno muafaka la human trafficking otherwise naungana na mtoa mada kwamba bajaji,tax,daladala,ndege n.k ni marufuku.
 
Kaka zangu, mbona mnaicheka Katiba yetu mpya? Nadhani si nidhamu nzuri kuicheka rasimu adhimu iliyoandikwa na weledi wa Taifa letu.

Sio masuala ya kusafirisha binadamu?

Utasemaje sio masuala ya kusafirisha binadamua wakati wao wenyewe wamesema "Biashara ya kusafirisha binadamua ni marufuku katika Jamhuri ya Muungano."??

Niko kwenye viroba na sikusoma vizuri?

Inawezekana aliyeandika katiba anajua kwamba anawaandia watu wenye upembuzi wa ki-viroba viroba, ambao hawana umakini wa kuyapa uzito masuala ya kisheria na kikatiba, unaweza ukawaandikia kitu chochote cha kilevi levi halafu anaeona tatizo ndio anaambiwa amekunywa viroba. Zingatia hilo.

WEWE ndio unatafsiri hivyo. MIMI niruhusiwe pia haki ya kutafsiri na kujadili kwa mujibu wa yaliyoandikwa. WAO wamesema: "Biashara ya kusafirisha binadamu ni marufuku katika Jamhuri ya Muungano."

Kwa hiyo Bodaboda, Bajaji, Daladala, Taxi, Pantoni za vivukoni, Gari Moshi, Ngalawa za kulipia, sasa marufuku.

unajitahidi kujenga hoja ila kwa akili za kawaida kweli warioba na timu yake wanaweza kumaanisha hivyo?..kodi itoke wap?...how abt self employment inayopigiwa kelele kila siku,watch out bro,usitumie tafsri sisisi.
 
Good point, wabadilishe lugha hapo, isije kutuletea balaa huko mbeleni.
 
RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2013

IBARA YA 25 ( 2 )

"Biashara ya kusafirisha binadamu ni marufuku katika Jamhuri ya Muungano."

Dukuduku langu: Wamiliki wa vyombo vya usafiri wa umma wanaotegemea sekta hii adhimu na
wananchi tusio na vyombo binafsi vya usafiri tutaishije katika enzi za Katiba mpya?

mkuu tuheshimiane tafadhari.
 
Kuwa makini na biashara za watu kijana!
Tunasomesha kwa hiyo kazi!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom