Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
Kwneye mchoro wa barabara hizo reserve zilikuwa kwaajili ya kupikia maandazi?Waache watu wafanye kazi
Hapo si kutumia fujo wala nguvu watembeze matangazo na elimu mara kwa mara hatari na athari za kufanya biashara maeneo hayo zifahamike kwa wavamiaji.View attachment 3615018
Wimbi la uvamizi wa hifadhi za barabara (road reserve) jijini Dar es Salaam linazidi kushamiri, huku wafanyabiashara, mama lishe, na madereva wa bodaboda wakikiuka sheria kwa kufanya biashara na kupita kwenye maeneo hayo. Tabia hii inachangia uharibifu wa miundombinu, ongezeko la ajali, na msongamano mkubwa.Vipaumbele vya Uvamizi wa Hifadhi za Barabara jijini:
Wafanyabiashara na Mama Lishe: Maeneo mengi ya wazi kando ya barabara (hifadhi) yamegeuzwa kuwa masoko na vizimba vya kupikia vyakula kama mihogo na maandazi. Moshi na uchafu unaotokana na shughuli hizi huchafua mazingira na kuhatarisha afya za watumiaji wa barabara.Ukipita magomeni usalama, road reserve bodaboda anakupigia honi uingie main road, ukingia mwendokasi bodaboda wanakupigia honi uwapishe yaani ni fujo. Madereva wa Bodaboda: Ili kukwepa msongamano wa magari katika njia kuu, madereva wengi wamekuwa na tabia ya kuacha barabara ya lami na kuingia kwa kasi kwenye hifadhi za barabara na barabara za waenda kwa miguu (service roads). Hali hii inahatarisha maisha ya watembea kwa miguu na kuharibu kingo za barabara.Hatua Zisizochukuliwa na Serikali:
Mamlaka za Jiji la Dar es Salaam zikishirikiana na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) zimeshindwa kuendesha misako ya mara kwa mara kuwaondoa wavamizi hawa na kutoa elimu kwa jamii ili kulinda miundombinu. Sheria za nchi zinakataza matumizi ya hifadhi ya barabara kwa shughuli za kiuchumi au usafiri binafsi bila vibali maalum.
Yard za Magari Wanayatoa ndai wanapaki kwenye reserve.Ni kosa ila lishahalalishwa,sijui kiongozi gani atakuja zuia hiki kitu
Tatizo itakuwa ni nini?Huu ujinga huwezi kuuona Rwanda
Uongozi wa hovyo, solution ni ndogo sana hapo, tunga sheria kama hazipo then enforce itTatizo itakuwa ni nini?
vinana wa UVCCM ndio wanao ombga hayo maeneo wanapanga biashara barabarani.Hapo si kutumia fujo wala nguvu watembeze matangazo na elimu mara kwa mara hatari na athari za kufanya biashara maeneo hayo zifahamike kwa wavamiaji.
Pili maeneo yale ambayo bado hayajavamiwa yalindwe na migambo wa jiji au halmashauri
Zaid waliovamia wapewe muda week tatu kusepa
Sheria zipo man, una enforce vipi wakati huyo mtu nyumbani kwake ndio kazungusha fremu mpaka chumba chake kulala?Uongozi wa hovyo, solution ni ndogo sana hapo, tunga sheria kama hazipo then enforce it
Matangazo ya mabango hayawezi kumtoa mtu ktk hayo maeneo. Labda mgambo.Hapo si kutumia fujo wala nguvu watembeze matangazo na elimu mara kwa mara hatari na athari za kufanya biashara maeneo hayo zifahamike kwa wavamiaji.
Pili maeneo yale ambayo bado hayajavamiwa yalindwe na migambo wa jiji au halmashauri
Zaid waliovamia wapewe muda week tatu kusepa
Mkuu namiini watu wa chama ndio wazuri na ni watu wa hamasa hao ilipaswa kuwa mfano kwa serikali na huyo DC kuwaelekeza katika maeneo tengefu. Lkn kama chama ambacho kinaunda serikali kimeamua kuchafua jiji lionekane jiji la hovyo basi hatutafika popotevinana wa UVCCM ndio wanao ombga hayo maeneo wanapanga biashara barabarani.
Pale Kinondoni kwa mkuu wa Wiulaya Machinga wamepanga biashara na zinalala hapo hapo kwenye mataa na DC yupo na hawaguswi, si mchezo!
Zaid hata wajeda wa jkt hawana kazi huko makambini wanakura viporo na kuvumbirwa kuota vitambi wapeni per diem mwez mmoja full time wamesambazwa katika hayo maeneo.Matangazo ya mabango hayawezi kumtoa mtu ktk hayo maeneo. Labda mgambo.
Serikali ya Samia yatenga Tzs trillion 1 kwa ajili ya safari za viongoziWaache watu wafanye kazi
Magomeni Mviringo ile open space wamegawana vijana wa UVCCM, wamejenga vibanda vya kudumu, Car WAsh, Bar na magenge ya kuza viroba , hivi kuna siku watakuja kuondolewa na kuna udharura gani watu kujenga baa eneo la wazi alafu mnataka taifa stars iingie WEDI KAP?Mkuu namiini watu wa chama ndio wazuri na ni watu wa hamasa hao ilipaswa kuwa mfano kwa serikali na huyo DC kuwaelekeza katika maeneo tengefu. Lkn kama chama ambacho kinaunda serikali kimeamua kuchafua jiji lionekane jiji la hovyo basi hatutafika popote