Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,290
- 2,468
Hii picha nimeitoa mtandaoni
Ipo changamoto inayoonekana kwa sasa kukua kwa kasi sana na ambayo isipofanyiwa kazi mapema basi tutakuwa na watoto/vijana wengi wenye matatizo ya kifua. Kwa sasa wimbi la bodaboda limeshika kasi. Ndio usafiri wa watu wa kati katika kuwahi shughuli zao za kila siku. Kama tunavyojua unapopanda kwenye huu usafiri, mwili wako unakuwa nje, na lolote linaweza kutokea, iwe ajali au maradhi kama mafua, kikohozi, na hata pneumonia.
Mimi ni mwendeshaji wa pikipiki. Wakati fulani nyuma huko niliwahi kupatwa na huu ugonjwa wa pneumonia. Ulinitesa sana. Ni kutokana na baridi kupiga kifuani na usoni hasa pale ambapo hujajikinga vyema.
Sasa kuna hawa watoto ambao wameanza chekechea. Wengi pia utakuta shule zao ziko mbali, na kusema wazazi watumie usafiri wa umma ni kwamba mtoto atachelewa. Wakisema mtoto atumie basi la shule, ni kwa wale wenye uwezo, na shule zenye aina hiyo ya usafiri. Hivyo basi kuna kundi la wazazi wameingia makubaliano na madereva wa boda boda kwa lengo la kuwapeleka watoto wao mashuleni asubuhi na kuwafuata mchana au jioni.
Ieleweke kwmba watoto hawa ni kati ya miaka minne hadi kumi hivi. Sasa kwa usalama ni kwamba dereva wa bodaboda humuweka mbele yake kama inavyoonekana kwenye picha hapo. Mtoto hana kinga yoyote usoni wala mwilini. Tena kwa nyakati za asubuhi hali ya hewa huwa na ubaridi sana. Pia ukiongezea na mwendo wa madereva hawa wa bodaboda njiani basi inakuwa tabu sana.
Njiani wiki kama mbili nikiwa nami kwenye pikipiki yangu dereva wa bodaboda akawa kampakiza mama mmoja ambaye alikuwa na watoto wawili. Mmoja kakaa nae na mwingine yuko mbele ya dereva. Ilibidi kuongeza mwendo ili nimfikie yule dereva na kumpa ishara kuwa huyo mtoto hapo mbele anaathiriwa na upepo. Watafute namna ya kumkinga. Mama yake anatoa macho tu. Dereva wa bodaboda kama alinielewa akachukua begi kama la shule na kumuwekea kifuani lakini inavyoonekana ni kama halikukaa vizuri. Nadhani aliliondoa. Mimi nikaongeza mwendo, la msingi ujumbe niliwafikishia.
SIku tatu tena hivi zimepita nikamwona dereva wa bodaboda kampakiza mtoto wa miaka minne hivi mbele. Japo kavaa sweta, bodaboda ilikuwa kasi sana kiasi unaona kabisa mtoto anapata shida kutazama mbele. Bado kwa sweta lile na mwendo ule ni ngumu kumkinga mtoto na athari za upepo hasa ukitegemea umri wao.
Kwa mwendo huu tunatengeneza janga lingine. Nashauri pawepo na taratibu zinazoeleweka za usafiri wa vyombo hivi hasa linapokuja suala la watoto. Ikiwezekana pawepo na helmet za watoto, lakini pia wazazi wahahikishe watoto wao wanakuwa salama katika vyombo hivi. Ni ngumu kuzuia vyombo hivi kutumika ila ni rahisi kudhibiti matumizi na kujali wengine pale wanapotumia vyombo hivi.
Nasisitiza kwa wazazi, wasiangalie tu mtoto kuwahi shule. Wahakikishe usalama wa watoto wao wanapokuwa wanaenda shule. Unaweza kufurahia mtoto kuwa anawahi lakini baada ya muda ukaanza kuwa mhudhuriaji mzuri wa mahospitali. Tuwe makini.
Updates: Hiyo clip nimeiweka hapa baada ya kuiona mitandaoni. Hii inakuja baada ya kuwa tayari nimewekahili bandiko hapa, hivyo waandaaji wa huu mchakato jaribuni kufanyiakazi nilichosemakwenye post yangu chini huko
Attachments
Upvote
8