Bodaboda nyingi za Kibaha hazina Side mirrors

Bodaboda nyingi za Kibaha hazina Side mirrors

godson njamakuya

Senior Member
Joined
Mar 6, 2021
Posts
170
Reaction score
196
Polisi wa Usalama barabarani inabidi wafuatilie ili kubaini ni kwanini pikipiki nyingi za Kibaha hazina Side mirror.

Utafiti mdogo nilioufanya baada ya kuwahoji baadhi ya madereva wa bodaboda walieleza kwamba wengi wameondoa vioo hivyo kwa madai kwamba, magari yanapokuwa kwenye foleni na wao wanapojaribu kupenya penya, side mirror za pikipiki zao hukwangua rangi kwenye magari ya watu na kusababisha kulipishwa fedha kutokana na uharibifu huo.

Ni sababu ambazo hazina uzito kama usalama wa maisha yao na abiria wao.
 
Itakuwa hautokagi nje ya Kibaha wewe hilo suala ni karibu Tanzania nzima mijini na vijijini mtu ananunua pikipiki mpya ikipita mwezi anafungua side mirrow zote.
 
Ila tuacheni utani, hizi side mirror huwa wanazipeleka wapi?
 
magari yanapokuwa kwenye foleni na wao wanapojaribu kupenya penya, side mirror za pikipiki zao hukwangua rangi kwenye magari ya watu na kusababisha kulipishwa fedha
Huo ni uongo
  1. Mishikio ya usukani ndiyo ingetajwa kwa hilo maana imejitokeza nje zaidi
  2. Hiyo penyapenya ipo vijijini? Mbona nako wanang'oa side mirror
  3. Wakifanya uharibifu wanatoroka ni ngumu kuwakamata hizo fedha wanatozwa na nani
 
Polisi wa Usalama barabarani inabidi wafuatilie ili kubaini ni kwanini pkpk nyingi za Kibaha hazina Side mirror.Utafiti mdogo nilioufanya baada ya kuwahoji baadhi ya madereva wa bodaboda walieleza kwamba wengi wameondoa vioo hivyo kwa madai kwamba, magari yanapokuwa kwenye foleni na wao wanapojaribu kupenya penya, side mirror za pikipiki zao hukwangua rangi kwenye magari ya watu na kusababisha kulipishwa fedha kutokana na uharibifu huo. Ni sababu ambazo hazina uzito kama usalama wa maisha yao na abiria wao.
Hili ni tatizo la nchi nzima. Na hata side mirror kwa pikipiki hizi za mchina zinazotumika kama bodaboda zimewekwa kama mapambo tu maana ziko chini mno kiasi cha mtumiaji hasa akiwa na kimo kirefu kupata tabu kuitumia, sijui walijipima wao!.
 
Polisi wa Usalama barabarani inabidi wafuatilie ili kubaini ni kwanini pkpk nyingi za Kibaha hazina Side mirror.Utafiti mdogo nilioufanya baada ya kuwahoji baadhi ya madereva wa bodaboda walieleza kwamba wengi wameondoa vioo hivyo kwa madai kwamba, magari yanapokuwa kwenye foleni na wao wanapojaribu kupenya penya, side mirror za pikipiki zao hukwangua rangi kwenye magari ya watu na kusababisha kulipishwa fedha kutokana na uharibifu huo. Ni sababu ambazo hazina uzito kama usalama wa maisha yao na abiria wao.
Huo ni uongo wa wazi wazi, side mirro zinaishia karibia sawa ya upana wa ule usukani.
Hao wanaotoa side mirrow ni watu ambao hawatambui dhamani ya maisha yao au niseme hawana leseni au wana leseni feki za kuendeshea hizo vyombo
 
Mmojawapo huyo hapo niliongozana naye jana

20211015_091202.jpg
 
Back
Top Bottom