voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,545
- 11,935
Hawana tofauti na zile kampuni za kukodishwa kulia na kuomboleza misibani!
Ambao huweza kulia kwa machozi tosha,ilhali hata Marehemu mwenyewe hawakuwahi kumuona kavla ya kufariki. Achilia mbali hata unasaba!
Kwao Boda oda, huangalia ujazo wa matenki ya Pikipiki(Bodaboda) zao! Wako tayari kutumika na chama chochote cha siasa, ilimradi mshiko wao uwepo tu.
Kwenye kipindi cha Kampeni, bodaboda mmoja,anaweza Participate misafara ya vyama tofauti hata vitatu kwa siku moja!
Hawajali kuhusu sera,hoja wala uelewa wa kile wanachokwenda kukiandamani,wao ni sera ya kujaziwa Mafuta tu.
Baada ya kufika eneo husika, huwa hawasubiri kusikiliza, hoja au sera za yule aliyewajazia Mafuta.
Huwa wanawahi vituoni kwao,ili wakayatumie yale Mafuta na kupata pesa zao.
Hoja yangu,wanasiasa wenye mtindo wa kuwajazia mafuta bida boda,wajuwe huwa wameliwa!
Na pia waelewe kwamba wananchi wanajua huo mchezo,kwa hiyo,huwa haileti ushawishi wowote kwa mwananchi kuweza kuhadaika!
Labda kwa vyama ambavyo huwa vina chukua video clips na kutuma kwa wafadhili wao,kuwahadaa kwamba wana uungwaji mkono kindakindaki,ilhali ukweli ukiwa tofauti.
Ndio maana nimewafananisha na wajumbe wa chaguzi mbalimbali za CCM,ambao hupokea pesa toka kwa kila mgombea huku wakimuhadaa kwamba wako nyuma yake mpaka kieleweke. Mwisho wa siku huwa ni kumbwaga chali mhusika
Jiwe hili ni kwa wanaohusika
Alamsikhi.
10101.