Bodaboda wanazeeka sana, ile kazi yao nahisi ni ngumu mno!

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Kuna dogo ni jirani yetu kijijini, nimempita kama miaka 12-15 Nilimwona miaka 5 imepita Kariakoo akifanya kazi kwa Wahindi na juzi nimemwona Kazini analeta bahasha akiwa na boda. Anasema aliacha kazi kwa Wahindi na kujiingiza kwenye ubodaboda.

Kijana kazeeka ghafla utadhani kanizidi umri. Kuna mwingine ni mdogo wangu one father, nimemwacha 2 yrs lakini unaweza kusema Mimi ni mdogo wake. Hii kazi ngumu sana, nahisi jua linawapausha mwili.

Bado nalia na Serikali, Serikali ijenge viwanda vingi vijana wapate ajira za kudumu huko viwandani. Bodaboda inaleta misiba na walemavu katika familia za maskini. Vijana wengi siku hivi wanakatwa miguu tu na kuwa mizigo kwa ndugu.

Pia soma=> Ukweli usemwe vijana wapone, bodaboda si ajira ni mtego
 
Binafsi napinga sana usafiri wa boda kurasimishwa na kupigiwa chapuo na wanasiasa kama suluhisho la ajira. Na pia huwa sipandi bodaboda; ningekuwa na mamlaka ningepiga marufuku!
CCM wameshaanza kuwapa vikoti vya picha ya Mama Samia
 
Halmashauri na miji waruhusiwe kuajiri vibarua kazi za kupanda miti, majani, maua, usafi mitaani,kujenga barabara na mitaro etc
 
Boda wanavuta hewa chafu mingi sanaa, stress njiani /kazini, in short hawatumii nyenzo muhimu za kutunza afya zao wawapo kazini na kula lishe boraa ---- baadhi wanashindia k-vant / smart-G etc
 
Jumlisha energy drinks, na kuvuta yale mafuta kwenye tank masaa yote.
Kwa namna moja kuna wachache waliokomaa wanalisha familia zao, mbali na hawa wala shada na majani, hapa arusha ni kero.
 
Kuna dogo ni jirani yetu kijijini, nimempita kama miaka 12-15 Nilimwona miaka 5 imepita Kariakoo akifanya kazi kwa Wahindi na juzi nimemwona Kazini analeta bahasha akiwa na boda. Anasema aliacha kazi kwa Wahindi na kujiingiza kwenye ubodaboda.

Kijana kazeeka ghafla utadhani kanizidi umri. Kuna mwingine ni mdogo wangu one father, nimemwacha 2 yrs lakini unaweza kusema Mimi ni mdogo wake . Hii kazi ngumu sana, nahisi jua linawapausha mwili.

Bado nalia na serikali, serikali ijenge viwanda vingi vijana wapate ajira za kudumu huko viwandani. Bodaboda inaleta misiba na walemavu katika familia za maskini. Vijana wengi siku hivi wanakatwa miguu tu na kuwa mizigo kwa ndugu.

Pia soma:Ukweli usemwe vijana wapone, bodaboda si ajira ni mtego
Kiwanda usisubiri serikali...anzisha wewe mdogo mdogo usaidie jamii
 
Hao wanatumia pombe kali...double kick, kuka n.k..
Ambao hawatumii hivyo vitu wamenawili tena mabishoo wanakula wake za watu tu
 
Kuna dogo ni jirani yetu kijijini, nimempita kama miaka 12-15 Nilimwona miaka 5 imepita Kariakoo akifanya kazi kwa Wahindi na juzi nimemwona Kazini analeta bahasha akiwa na boda. Anasema aliacha kazi kwa Wahindi na kujiingiza kwenye ubodaboda.

Kijana kazeeka ghafla utadhani kanizidi umri. Kuna mwingine ni mdogo wangu one father, nimemwacha 2 yrs lakini unaweza kusema Mimi ni mdogo wake. Hii kazi ngumu sana, nahisi jua linawapausha mwili.

Bado nalia na Serikali, Serikali ijenge viwanda vingi vijana wapate ajira za kudumu huko viwandani. Bodaboda inaleta misiba na walemavu katika familia za maskini. Vijana wengi siku hivi wanakatwa miguu tu na kuwa mizigo kwa ndugu.

Pia soma=> Ukweli usemwe vijana wapone, bodaboda si ajira ni mtego
Boda wengi hawajitunzi, uchafu, ulevi, bangi na mapenzi kwa sana. Wakirekebisha hayo hata mengine yatawezekana. Ila hoja ya kuchakaa sio kwa boda tu, yapo makundi mengi kwenye hili.
 
Back
Top Bottom