Bodaboda zinatumaliza, abiria na madereva tuwe makini

Bodaboda zinatumaliza, abiria na madereva tuwe makini

Tupate picha kidogo
 
Attachments

  • GKzlovkX0AIBz66.jpeg
    GKzlovkX0AIBz66.jpeg
    125.7 KB · Views: 5
Bodaboda hazikupaswa kuwa chombo cha kupakia abiria kibiashara...

Ujonga wa wanasiasa kama kawaiida umetufikisha kwenye hii kadhia...
Si muache kuzitumia au wanasiasa wanashikia watu fimbo wapande? Humu huwa nasema mimi sipandi bodaboda lakini kuna watu povu linawatoka wanasema najidai sijui naringa upuuzi mtupu. Kwani kabla bodaboda kuingia tulikuwa tunafikaje tuendako?
 
Boda ni tatizo kubwa sana.

Ila vijana wengi mno wamo huko aisee.

Kwa Dar pia bajaji nayo inafuatia nyuma ya Boda kwa kujaza vijana wengi halafu wanafanya uhuni huko balaa.
 
Si muache kuzitumia au wanasiasa wanashikia watu fimbo wapande? Humu huwa nasema mimi sipandi bodaboda lakini kuna watu povu linawatoka wanasema najidai sijui naringa upuuzi mtupu. Kwani kabla bodaboda kuingia tulikuwa tunafikaje tuendako?

Mwananchi mmoja kuacha kutumia bodaboda ni uamuzi binafsi ambao kwa namna moja au nyingine unaweza usiwe na matokeo makubwa kama ambavyo serikali ikiamua kuweka zuio...
 
Mwananchi mmoja kuacha kutumia bodaboda ni uamuzi binafsi ambao kwa namna moja au nyingine unaweza usiwe na matokeo makubwa kama ambavyo serikali ikiamua kuweka zuio...
Kuna bodaboda wenye akili zao,wanaendesha maisha yao kwa kazi hio. Kuna bodaboda wenye akili zao wanatusaidia sana kwenye delivery ya mizigo. Sasa upige marufuku bodaboda kwasbaabu ya wendawazimu fulani? Ni kama kupandisha bei mafuta ya taa kisa yanatumika kuchakachua diesel.
 
Kuna watu wanajifunza kwa kusikia,(Hawa wanakuwa salama)
Kuna watu wanajifunza kwa kuona(Baada ya majanga).

Kwenye kundi la pili, ni kwamba kila siku tuwe tunazika watu ndio akili itakaa sawa, na kuja kuwa watu wa kundi la kwanza.
 
Kuna bodaboda wenye akili zao,wanaendesha maisha yao kwa kazi hio. Kuna bodaboda wenye akili zao wanatusaidia sana kwenye delivery ya mizigo. Sasa upige marufuku bodaboda kwasbaabu ya wendawazimu fulani? Ni kama kupandisha bei mafuta ya taa kisa yanatumika kuchakachua diesel.

Kama ni delivery au usafiri basi urasimishwe, na ruksa ya kuziweka bodaboda kama sehemu ya uchukuzi iwe ni kwa mfumo wa kampuni na sio holela kama ilivyo sasa...

Kinachosumbua kwa sasa ni namna ya udhibiti, zimeachwa tu kuwa holela pasipo kuzingatia suala la bima, wapi zipite na wapi zisipite, muda gani zifanye kazi na muda upi zizuiwe n.k
 
Ukipanda boda halafu akingia highway njia panda au makutano ya barabara za mjini..kukuponza ni asilimia kubwa.
Wengi wanakua na over confidence,sijui sabbu Wana speed na kupenya ni rahisi?
 
Serikali ipige marufuku bodaboda kwenye barabara kuu, uwe usafiri wa mitaani na pembezoni mwa miji tu.
 
Kwa sasa bodaboda na bajaj ni heri bodaboda, bajaj zimekuwa za hovyo sana.
 
Back
Top Bottom