Bodi wamehairisha derby kusubiri uchunguzi, hapohapo watatangaza siku ya kurudiwa mechi. Kama ushatangaza marudio uchunguza wa nini kama sio uhuni?

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
BODI hii imejaa wahuni sana sana sijui tunaelekea wapi. Hawa jamaa ukisoma barua zao wanasema wamehairisha kwa sababu ya uchunguzi.

Hapohapo wanasema watatangaza siku nyingine ya marudiano.

Kama mmeshaamua kurudiwa unachunguza nini? huu ni ushenzi na uhuni si mngesema tu tumehairisha kwaajili ya simba.

Shame on you Kassongo.
Shame kwa BODI yako.
Shame on you TFF.
 
MCHANGO WANGU KAMA MWANA MICHEZO

1 Nafikiri ni muda sasa wa kupitia upya Kanuni zinazoongoza mpira wetu TANZANIA

2 Vitendo visivyo vya kiungwana na vinavyovunja kanuni zetu vimezoeleka kiasi cha watu kuhisi ni kawaida kufanyika na havtiliwi maanani.

3 Hata ukiwasikiliza watu mifano wanayotoa ni kwamba mbona kanuni hii ilivunjwa Mwanza katika mchezo wa SIMBA dhidi ya PAMBA na bado mchezo ukachezwa ?

4 Nafikiri kadhia hii SIMBA anakutana nayo kwa mara ya tatu Mchezo dhidi ya PAMBA lakini pia kuna siku SIMBA ana mechi uwanja wa KMC .

5 Mimi nafikiri lingekuwa ni jambo la ajabu sana SIMBA kukubaliana na kitendo kilichofanyika pale Taifa juzi hasa kwenye mechi Muhimu ya msimu.

6 Kuna wakati munatakiwa kurekebisha makosa kwa maumivu kama haya .

SIMBA ni club kubwa barani Afrika inapaswa kujipa heshima kwanza yenyewe kabla wengine kuiheshimu .

7 Huwezi kuwasimamisha wachezaji wa masaa MATATU nje ya geti la uwanja wachezaji ambao kwanza wanagharama kubwa lakini wapo kuelekea mchezo Muhimu wa msimu.

8 Walichokifanya SIMBA ni fundisho kwa club zinazodhani kila timu ni ya daraja la kuchezewa.

9 Na wanachokitaka SIMBA ni kujua nyuma ya huu upuuzi kuna kina nani ?

Na hawa ndo watu wanaoharibu mpira wetu na wengine wapemewa dhamana ya kutuletea maendelea wamejisahau wamelewa na ushabiki wa mpira.
 
Mpira wa nchi hii unaharibiwa kwa vitu vikuu vifuatavyo
1. Imani za kishirikina
2.kupanga matokeo hasa kwa yanga.
3.Bodi dhaifu
4.siasa kuongilia mpira.
 
MCHANGO WANGU KAMA MWANA MICHEZO

1 Nafikiri ni muda sasa wa kupitia upya Kanuni zinazoongoza mpira wetu TANZANIA

2 Vitendo visivyo vya kiungwana na vinavyovunja kanuni zetu vimezoeleka kiasi cha watu kuhisi ni kawaida kufanyika na havtiliwi maanani.

3 Hata ukiwasikiliza watu mifano wanayotoa ni kwamba mbona kanuni hii ilivunjwa Mwanza katika mchezo wa SIMBA dhidi ya PAMBA na bado mchezo ukachezwa ?

4 Nafikiri kadhia hii SIMBA anakutana nayo kwa mara ya tatu Mchezo dhidi ya PAMBA lakini pia kuna siku SIMBA ana mechi uwanja wa KMC .

5 Mimi nafikiri lingekuwa ni jambo la ajabu sana SIMBA kukubaliana na kitendo kilichofanyika pale Taifa juzi hasa kwenye mechi Muhimu ya msimu.

6 Kuna wakati munatakiwa kurekebisha makosa kwa maumivu kama haya .

SIMBA ni club kubwa barani Afrika inapaswa kujipa heshima kwanza yenyewe kabla wengine kuiheshimu .

7 Huwezi kuwasimamisha wachezaji wa masaa MATATU nje ya geti la uwanja wachezaji ambao kwanza wanagharama kubwa lakini wapo kuelekea mchezo Muhimu wa msimu.

8 Walichokifanya SIMBA ni fundisho kwa club zinazodhani kila timu ni ya daraja la kuchezewa.

9 Na wanachokitaka SIMBA ni kujua nyuma ya huu upuuzi kuna kina nani ?

Na hawa ndo watu wanaoharibu mpira wetu na wengine wapemewa dhamana ya kutuletea maendelea wamejisahau wamelewa na ushabiki wa mpira.
Kanuni zipo wazi, hakuna kanuni ya kuahirisha mechi hapo. Bodi ya ligi ni wahuni tu, kama Simba walizuiliwq kwa nini bodi haikudhiazibu timu husika. Hao viongozi wa bodi hawastahili kuwa hapo walipo. Ila Simba nao waoga hawana timu ya kupambana na Yanga ndiyo maana wamekimbia.
 
Shida ya hii nchi yetu ni kuruhusu siasa kutawala kila mahali. Badala ya kuwekeza kwenye maarifa, maadili, uwajibikaji, uzalendo, nk. Sisi tumeipa nafasi siasa itawale kila sehemu.
 
Back
Top Bottom