MCHANGO WANGU KAMA MWANA MICHEZO
1 Nafikiri ni muda sasa wa kupitia upya Kanuni zinazoongoza mpira wetu TANZANIA
2 Vitendo visivyo vya kiungwana na vinavyovunja kanuni zetu vimezoeleka kiasi cha watu kuhisi ni kawaida kufanyika na havtiliwi maanani.
3 Hata ukiwasikiliza watu mifano wanayotoa ni kwamba mbona kanuni hii ilivunjwa Mwanza katika mchezo wa SIMBA dhidi ya PAMBA na bado mchezo ukachezwa ?
4 Nafikiri kadhia hii SIMBA anakutana nayo kwa mara ya tatu Mchezo dhidi ya PAMBA lakini pia kuna siku SIMBA ana mechi uwanja wa KMC .
5 Mimi nafikiri lingekuwa ni jambo la ajabu sana SIMBA kukubaliana na kitendo kilichofanyika pale Taifa juzi hasa kwenye mechi Muhimu ya msimu.
6 Kuna wakati munatakiwa kurekebisha makosa kwa maumivu kama haya .
SIMBA ni club kubwa barani Afrika inapaswa kujipa heshima kwanza yenyewe kabla wengine kuiheshimu .
7 Huwezi kuwasimamisha wachezaji wa masaa MATATU nje ya geti la uwanja wachezaji ambao kwanza wanagharama kubwa lakini wapo kuelekea mchezo Muhimu wa msimu.
8 Walichokifanya SIMBA ni fundisho kwa club zinazodhani kila timu ni ya daraja la kuchezewa.
9 Na wanachokitaka SIMBA ni kujua nyuma ya huu upuuzi kuna kina nani ?
Na hawa ndo watu wanaoharibu mpira wetu na wengine wapemewa dhamana ya kutuletea maendelea wamejisahau wamelewa na ushabiki wa mpira.