Bodi ya Chelsea yamjadili Mourinho

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,701
Reaction score
1,714
Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich amekutana na bodi ya klabu hiyo kujadili hatima ya meneja wa klabu hiyo Jose Mourinho.


Hii ni baada ya klabu hiyo kuandikisha matokeo mabaya sana msimu huu, matokeo ya karibuni zaidi yakiwa kuchapwa 2-1 na Leicester ligini Jumatatu.


Hiyo ilikuwa mara ya tisa kwa Chelsea kushinda Ligi ya Premia katika mechi 16 na sasa wamo alama moja pekee juu ya eneo la kushushwa daraja.


Haijabainika iwapo Mourinho, 52, bado atakuwa kwenye usukani wakati wa mechi kati ya The Blues na Sunderland Jumamosi uwanjani Stamford Bridge.


Abramovich alitangaza kwamba bado alikuwa akimuunga mkono Mourinho Oktoba lakini matokeo hayajaimarika.


Abramovich na wenzake uongozini Chelsea wamekuwa wakimuunga mkono meneja huyo lakini kuna kizungumkuti cha ni hadi lini watasubiri klabu hiyo iimarike.


Tatizo jingine ni kwamba kwa sasa hakuna meneja msifika ambaye hana kazi na anaweza kuitwa upesi kujaza pengo.


Carlo Ancelotti ambaye hana kazi tayari alikuwa Chelsea awali na akafutwa.


Meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola na Diego Simeone Atletico Madrid bado wana majukumu kwa sasa.


Hili limepelekea uvumi kwamba sasa huenda Chelsea ikarudi tena kwa Guus Hiddink kwa mkataba wa muda.


Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 69 alishikilia usukani kwa muda Chelsea mwaka 2009 na kuongoza klabu hiyo kushinda Kombe la FA.
 
Wamuache kwanza...huyu morinho ana maajab mengi ktk soka na usishangae akachkua UEFA kama mzaha...Pia naomba niulize hv yule jamaa aliyewahi kuwa kocha msaidizi na kuachiwa timu dk za mwisho na Boas kisha akaukwa u'UEFA hv yupo wapi na je ana kibarua kwa sasa?
 
Bodi imuache uyu domo kaya amalize msimu ni buradani kuona akiwa humiliated ni vema akazama na chombo huku tukimuona na imani itamfanya awe na heshima maana makocha wenzie mostly wako kimya hakuna anaemnanga,nafikiria balaa lake ndio lingekua la Wenger au Van Gaal lazima angepayuka na bado namuombea vipigo mfululizo.
 

Unachanganya madesa wewe,aliechukua UEFA sio Boas.
 

Robert de mateo alienda ujerumani kwenye klabu ya schalk 04 kuna kipindi,alikua na wakati mgumu ktk bundersliger akafukuzwa, kwasasa yupo huru ila anaweza kwenda swansea au lazio
 
Tugempata gadiola au Diego simone tungesumbua
 
Mourinho tayari, kwisha habari yake
 
i would like this suprise move: MUFC run for Mourinho now, weka mkataba haraka wa kuanza kazi Januari 2016. Mpe hela nyingi akale Asia while pouring down the burden has been struggling with Chelsea and get new ideas.

What are you waiting Ed?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…