Waundaji maudhui (content creators) wanaoripoti habari na kufanya mahojiano wametakiwa kupata kibali cha uandishi wa habari (accreditation) ili kufuata sheria
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Wanahabari (JAB), Bw. Patrick Kipangula, alisema mtu yeyote anayefanya kazi za kihabari bila kuwa na ithibati/kibali anaweza kuwa anavunja sheria.
"Chini ya Kifungu cha 19 cha Sheria ya Huduma za Habari, hakuna mtu anayeruhusiwa kufanya kazi ya uandishi wa habari bila kupata ithibati kutoka Bodi ya Ithibati ya Wanahabari," alisema.
Bw. Kipangula alieleza kuwa kazi za kihabari zinajumuisha kuripoti habari za kawaida na matukio ya sasa, pamoja na kufanya mahojiano (interviews). Hii ina maana kwamba content creators wanaofanya shughuli hizo wanatakiwa kufuata masharti ya kupata ithibati hiyo
Aliongeza kuwa ili kupata kibali hicho, mhusika anapaswa kukidhi vigezo vya kisheria, ikiwemo kuwa na angalau
Stashahada (Diploma) ya Uandishi wa Habari.
Hata hivyo, alitofautisha kati ya waundaji wa maudhui ya kawaida na wale wanaofanya kazi za uandishi wa habari:
"Kama unatengeneza maudhui yasiyo ya kihabari, sheria hiyo haikuhusu," alisema.
Bw. Kipangula alisema JAB inaendelea kuwafuatilia content creators wanaojihusisha na kazi za habari, na tayari imeshakaa na baadhi yao kujadili masharti hayo ya kisheria
Source: The Citizen