Bodi ya Kahawa (T) ni shirika la umma ambalo baadhi ya majukumu yake ni:-
· Kuishauri serekali juu ya kanuni bora za maendeleo ya zao la kahawa Tanzania
· Kushughulikia uzalishaji na usafirishaji wa kahawa ndani na nje ya Tanzania
· Kulinda maslahi ya wakulima wa kahawa katika kuuza kahawa yao ili wapate bei inayolingana na jasho lao
· Kuweka sera za uzalishaji, usafirishaji na utunzaji wa kahawa na mazao yatokanayo na kahawa
· Kuwakilisha Tanzania katika mikutano ya kimataifa ihusuyo kahawa nk.
Kwa jumla Bodi ya Kahawa ni chombo cha umma ambacho mkulima wa kahawa Tanzania anakitegemea kimtafutie soko zuri ili mkulima afaidike na kilimo cha kahawa. Kinyume chake inasikitisha kuona chombo hiki kimegeuka kuwa mwizi mkubwa wa wakulima wa kahawa badala ya kuwatetea na kuwalinda. Bodi imekuwa inawaibia wakulima kwa namna ambayo mkulima maskini wa Tanzania haelewi anavyoibiwa. Hata baada ya wachache wanaofahamu mbinu hizo chafu kupiga kelele kwenye vyombo vya serekali; kwa maana Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika; hawajasaidika.
Napenda nidokeze hapa kwa faida ya wakulima wa kahawa Tanzania na umma kwa jumla, hasa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na vyombo vingine vya serekali vinavyohusika; jinsi wizi huo unavyofanywa ili mkulima asaidiwe kupata malipo halali kwa jasho lake.
1. Bodi ya Kahawa Tanzania huendesha mnada wa kahawa katika soko lake lililoko Moshi (Moshi Coffee Exchange) kila siku ya Alhamisi (wakati wa msimu wa kahawa Julai- Februari.) Katika soko hili Bodi ya Kahawa husimamia mauzo ya kahawa kutoka kwa wanye kahawa (vikundi vya wakulima, vyama vya ushirika, wakulima binafsi au wakulima wenye mashamba makubwa). Bodi ya Kahawa inakuwa ni msimamizi wa kuhakikisha soko linaendeshwa kwa taratibu zinazokubalika kwani ndiyo dhamana waliyopewa na serekali. Mwenye kahawa (Muuzaji) anakabidhi mamlaka ya kuuza kahawa yake kwa Bodi ya kahawa (wakala wa muuzaji). Wanunuzi wawakishanunua kahawa wanatakiwa wailipe Bodi ya kahawa fedha za manunuzi kabla ya siku saba kuanzia siku walipoinunua mnadani.
2. Mauzo ya kahawa katika mnada hufanywa kwa Dola za Kimarekani. Hii ni kwa sababu wanunuzi wengi wanaoshiriki katika mnada huko wanawakilisha makampuni mbali mbali duniani. Kwa kutumia dola ya Kimarekani, inakuwa rahisi wanunuzi hao kutafsiri haraka manunuzi kwa sarafu za kampuni/nchi wanazoziwakilisha. Wanunuzi huilipa Bodi ya Kahawa kwa dola; na Bodi ya Kahawa huwalipa wenye kahawa zao kwa dola au kwa shilingi za Kitanzania kulingana na matakwa ya mwenye kahawa. Vyama vya Ushirika na wakulima wakubwa wa kahawa mara nyingi hupenda kulipwa kwa dola, lakini vikundi vya wakulima, na wakulima wadogo hupenda kulipwa kwa fedha za Kitanzania. Inapotokea mwenye kahawa anataka kulipwa kwa fedha za Kitanzania; Bodi ya kahawa hubadili dola alizopata mnadani na kumlipa kwa shilingi za Kitanzania. HAPA NDIPO MKULIMA HUIBIWA!
3. Siku ya mnada bodi ya kahawa hutoa kiwango elekezi cha kubadilisha dola (exchange rate) ili mwenye kahawa akadirie atapata kiasi gani kwa fedha za Kitanzania. Kwa muuzaji anayetaka kulipwa kwa fedha za Kitanzania, bodi ya kahawa hubadilisha dola za mauzo alizopata mnadani katika mabenki. Mara nyingi bodi inapewa viwango maalum (special rates); kwa kuwa wanabadilisha dola nyingi kwa mara moja. Badala ya bodi kumlipa muuzaji fedha kiasi kilichopatikana; badala yake bodi ya kahawa huwalipa kwa kiwango elekezi walichopewa siku ya mnada, na tofauti inakuwa ni faida kwa Bodi ya Kahawa. Bodi ya Kahawa inapata faida kubwa kwa kutumia mtindo huo kuwaibia wakulima; na hiki kimekuwa chanzo kimojawapo cha mapato kwa bodi hiyo.
Misimu mitatu 2009/10, hadi 2011/12 Bodi ya Kahawa imepata zaidi ya Shilingi 1.6 bilioni kutokakna na biashara hiyo haramu kama ifuatavyo:
[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 2009/2010[/TD]
[TD="width: 172"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 120"] 2010/2011[/TD]
[TD="width: 172"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 120"] 2011/2012[/TD]
[TD="width: 172"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 120"] JUMLA[/TD]
[TD="width: 172"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Takwimu hizi ni kwa mujibu wa hesabu zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serekali. Hesabu zinaonyeshwa ni "faida kutokana na ubadilishaji fedha" (gain on exchange rate.)
Ni ukweli kwamba
(i) Fedha zinazopatikana kutokana na kubadili fedha za mkulima wa kahawa ni za mkulima mwenye kahawa. Bodi imewasaidia kuzibadilisha tu. Bodi haitakiwi kufanya biashara na fedha za wakulima. Bodi ya kahawa kwa jinsi hii, inawahujumu wakulima wake.
(ii) Kwa kubadilisha fedha za wakulima kwa faida, Bodi ya Kahawa inafanya kazi kinyume na madhumuni ya kuundwa kwake. Bodi ya kahawa siyo Asasi ya Fedha.
(iii) Bodi ya kahawa imefanya biashara ya kubadili fedha na kupata faida kubwa ya 1.6 billioni kwa misimu mitatu; Je, bodi ya kahawa imeilipa serekali kodi kiasi gani?
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi aliyejiuzulu; Mama Hawa Sinare, pamoja na bodi yake ya Wakurugenzi walianza vizuri kwa kuhoji mambo mengi yanayolalamikiwa ikiwa ni pamoja na
(a) Kwa nini wakulima wanalipwa kwa mtindo kama ulivyoelezwa hapo juu; na
(b) Kero za wafanyakazi kulalamikia uongozi mbovu; kuangalia uwezekano wa kupunguza mrundikano wa kesi zilizoko mahakamani hasa zile zinazowahusu wafanyakazi. Kwa bahati mbaya sana Mwenyekiti huyo aliondolewa kabla hajafika mbali, kwa hila za mkurugenzi mkuu ndugu Mh. Eng. Adolph Kumburu akishirikiana na swahiba wake mbunge mmoja wa kusini. Walihakikisha wanatumia kila hila ili bodi ya wakurugenzi chini ya mama Sinare ibadilishwe kwani waliona hatari iliyokuwa mbele yao.
Mwisho
1.
(a) Waziri mwenye dhamana Mh. Eng. Christopher Chiza, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika; wakulima ni wadau wako. Fuatilia ukweli huu ili uwaokoe wakulima kutokana na wizi huu unaoongozwa na ndugu Adolph Kumburu. Mkulima ataendelea kuumizwa mpaka lini?
(b) Mkataba wa Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Kahawa ndugu Adolph Kumburu umemalizika tarehe 1 Oktoba 2013. Ndugu Kumburu anajitahidi kwa njia zote kuhakikisha anaendelea kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Mh. Waziri uelewe kwamba aliyofanya yanatosha; kuendelea kwa miaka mingine mitano ni majanga kwa wadau wote wa kahawa. Wakulima tunalia, wafanyakazi wanalia. Wafanyakazi wanasema manejimenti ya bodi ya kahawa ni Adolph, Murugenzi wa Fedha na mhasibu wake mmoja, hakuna zaidi ya hapo; tutafika kweli?
2. Bodi ya kahawa imepata faida ya shilingi 1.6 bilioni kutokana na biashara haramu ya kubadilisha fedha za wakulima. Mamlaka ya Mapato Tanzania inayo kodi ya kukusanya kutoka bodi ya kahawa kama bodi hiyo haitarudisha fedha hizo kwa wakulima husika.
TRA KUSANYA KODI!

[TD]
MSIMU
[TD]
TZS
[/TR]
[TR]
[TD] 2009/2010[/TD]
[TD="width: 172"]
551,426,000
[/TR]
[TR]
[TD="width: 120"] 2010/2011[/TD]
[TD="width: 172"]
855,139,000
[/TR]
[TR]
[TD="width: 120"] 2011/2012[/TD]
[TD="width: 172"]
202,659,000
[/TR]
[TR]
[TD="width: 120"] JUMLA[/TD]
[TD="width: 172"]
1,609,404,000