Bodi Ya Ligi fuatilieni fununu za mechi za matokeo ya kupangwa

Bodi Ya Ligi fuatilieni fununu za mechi za matokeo ya kupangwa

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Natumaini wana bodi nao huwa wanatazama hizi mechi hasa za Nbc Premier League. Najua na wao wanaona kama tuonavyo sisi, wanapata muda wa kutafakari, kuchambua kati ya pumba na mchele.

Basi tuombe kwa nafasi zao wasiishie kuguna guna, bali utokeapo utata na sintofahamu katika matokeo ya mchezo na maamuzi ya waamuzi tata wao kama bodi wafike mbali zaidi, ikiwezekana hata kuwatumia TAKUKURU ili kuunusuru mchezo wetu pendwa wa kandanda.

Na itapendeza itokeapo timu mbili zimehusika kwenye mchezo mchafu wa kupanga matokeo timu zote zipate adhabu ya kushushwa daraja, zikacheze ligi daraja la kwanza zigombee kurudi tena Premier.

Nayasema haya ili kuokoa mchezo huu, kuuletea heshima, lakini pia kuzipa changamoto timu zifanye maandalizi mapema, usajiri mzuri na si kushindwa kusajiri vizuri na mwishowe kuanza kutumia njia za ujanja ujanja kununua waamuzi na kuhonga wachezaji.

Bodi ya ligi hili mlitazame sasa.

Nawasilisha.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Makolokolo/Mbumbumbu/Malalamiko/Makelele/Kolowizards...wanakuja kukupopoa kwa kejeli na matusi kedekede.

Makolokolo wakishinda mechi zao "wako vizuri sana kisoka", wakishinda Yanga "bahasha zimetembea"....[emoji116][emoji28]
JamiiForums1586558777.jpg


Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Ngada FC, Sembe FC, Pusha FC hao ndo zao kwa bahasha.
 
Timu kubwa 16 Africa ziko Caf Cl, sasa inawezekanaje asiyeweza akawa huko?.
Tumieni .... kufikiri
Ngada FC, Sembe FC, Pusha FC wachunguzwe kwa kutumia msuba na poda.
 
Back
Top Bottom