kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kocha ni kama mzazi na mlezi wa wachezaji wake, wachezaji wanamtegemea kocha na nahodha wao wanapokuwa viwanjani.
Haiwezekani makocha wakae kimyaa kabisa kwa waamuzi wasiofanya haki kwa wachezaji na timu yake. Binadamu hayuko hivyo, kuna wakati anaweza kusema kitu bila kukusudia kutokana na ubaya, uzuri au ukubwa au hatari ya tukio.
Kuwanyamazisha makocha ni dalili mbaya sana kwa soka letu, maana hii itatoa mwanya kwa timu kununua mechi kupitia kwa waamuzi au waamuzi kuamua kwa kusukumwa na mahaba Yao kwa timu husika.
Kwanini timu zinazolalamikiwa ni zilezile za Simba na Yanga TU? Kwanini kadi nyekundu zinazinufaisha Simba na Yanga zaidi kuliko timu nyingine? Mfano, Simba ushindi wake msimu huu ulitegemea timu pinzani kupewa kadi nyekundu. Yanga ilipata goli dhidi ya ruvu kwa mchezaji kupewa kadi nyekundu ya utata. Mwamuzi anapewa ushauri na mchezaji mnufaika na aina ya adhabu kuhusu aina ya kadi ya kumpa mchezaji wa timu pinzani.
Hivi ni kweli kocha asipanue mdomo kunung'unikia mwamuzi mkora kiasi hicho? Kwani iwepo hata TV moja uwanjani ya kuisaidia replay na slow motion ya tukio lenye utata kiwanjani?