Bodi ya Ligi Kuu imewashirikisha Yanga kabla ya kutoa ratiba,ili wasiharibu ratiba kwa kujitoa?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi (TPLB) limetangaza ratiba mpya ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2018/19 itakayoanza Agosti 22 2018.

Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Boniface Wambura, amesema ligi hiyo itahusisha jumla ya mechi 380 kutoka 240 ambazo zilikuwa zilichezwa msimu uliopita kutokana na ongezeko la timu.

Wambura ameeleza katika msimu wa 2017/18 ligi ilihusisha jumla ya timu 16 pekee lakini kuelekea msimu ujao kutakuwa na idadi ya timu 20 ambazo zimefanya kuwe na ongezeko la idadi ya mechi.

Ratiba hiyo inaonesha mechi zitakazoanza Agosti 22 ni baina ya Simba SC dhidi ya Tanzania Prisons, Ruvu Shooting vs Ndanda FC, Singida United United dhidi ya Biashara FC, Alliance FC dhidi ya Mbao FC pamoja na Kagera Sugar watakaocheza na Mwadui FC.

Wakati huo mechi yenye msisimko mkubwa itakayowakutanisha watani wa jadi, Simba na Yanga, itachezwa Septemba 30 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ambapo Simba atakuwa nyumbani
 
Ahahaha we mtoa mada! Acha kuwandama Yanga wanzako walikua wanajiandaa na Kombe la shirikisho wakakacha hata Kagame saizi kinachowakuta uko Kenya siri yao, sasa ungewacha tu maumivu ya kichapo wanachokipata uko Ukija kuwachanganya na tarh 30 September utawafanya machungu yazidi
 
Swali lang n kuwa n utaratibu gan umetumika mpaka kuongeza tim kutoka 16 had 20
 
Mbumbumbu fc hakukosea aliyewaita hivyo
 
Vyura bhn speed ya 4G sion mchezo asee.[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
walijitoa kagame ili wapigwe 4g vizuri na gor mahia
 
Wangekwepo kwenye kagame wangefungwa na kila timu,aibu sana
 
Pale 4-0 ndio kajiandaa ina maana angeshiriki Kagame cup angepigwa zaidi ya goli nne(4)
 
mwenyekiti wetu ndio tajiri numero uno hapa TZ..sasa kuna wale waliokulia maisha ya kimasikini kijijini wanamuonea wivu...ila Mungu mkubwa walitaka afe kabisa..unamiliki TIGO 99% lazima wasande..anarudi Jangwani kwa kishindo hofu inatanda mpaka TFF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…