Bodi ya Ligi: VPL Kurejea Juni

Bodi ya Ligi: VPL Kurejea Juni

HPAUL

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2011
Posts
410
Reaction score
567
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi VPL amesema TFF inafanyia kazi maoni ya Mh. Rais Magufuli, na ligi itarejea Juni bila ya watazamaji.

======

ALMAS Kasongo, Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) amesema kuwa wanakwenda kuifanyia kazi kauli ya Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Jana, Aprili 3, Magufuli alisema kuwa anafikiria kurejesha ligi za Tanzania ambazo zilisimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Kasongo amesema Kamati ya Uongozi ya TFF imeazimia kuwa ligi iendelee kulingana na maelekezo ya Serikali na mechi zitachezwa bila mashabiki kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
 
Asalaam aleykum Dar es Salaam, Asalaam alyekum Tanzania, Asalaam alyekum afrika mashariki na dunia kote mnapotupata.

Mimi ni Baraka Mpenja sauti ya radi nikikuletea matangazo ya moja kwa moja kutoka uwanja wa taifa, pambano kati ya Simba "Mabingwa wa nchi" lunyasi wakichuana vikali na watoto wa kinondoni "Kino boys"

Uwezekano wa mvua kunyesha ni 5%.......



"Not everything is for everybody"
 
Bora irejee tu ili wale mbumbumbu fc wasipewe ushindi wa mezani. Wamebebwa na waamuzi weee! bado waendelee tena kubebwa na corona!!!
 
Usikose kuangalia kipindi cha Tamasha la Michezo ITV kuanzia saa nane mchana ili umshuhudie Kocha Liston Katabazi akieleza kwa undani madudu ya TFF na ubadhilifu wa pesa unaofanywa na viongozi wachumia tumbo wa shirikisho hilo ambao ndio chanzo cha kudumaa kwa mchezo wa Soka hapa nchini.
 
👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹
 
Back
Top Bottom