Bodi ya ligi yafanya mabadiliko madogo ratiba ya ligi kuu Tanzania Bara

qaxemvule

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
231
Reaction score
120
Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limefanya mabadiliko kidogo katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kama ifuatavyo.

Michezo ambayo imefanyiwa mabadiliko ni kati ya Tanzania Prisons na Majimaji ya Songea ambao utafanyika Septemba 5, 2017 wakati Septemba 6, mwaka huu Azam FC itacheza na Simba; Njombe Mji na Young Africans; Mtibwa Sugar na Mwadui FC.

Pia tarehe hiyo ya Septemba 6, mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Lipuli na Stand United; Singida United na Mbao; Kagera Sugar na Ruvu Shooting wakati Mbeya City na Ndanda FC .

Michezo mingine ambayo imesogezwa hadi Septemba 11, 2017 ni kati ya Azam na Kagera Sugar wakati Mbao na Tanzania Prisons utachezwa Septemba 21, mwaka huu.

Kadhalika mechi nyingine zitachezwa Oktoba 11, mwaka huu ni kati ya Mbao na Azam FC; Kagera Sugar na Mwadui; Mbeya City na Ruvu Shooting; Ndanda na Singida United.

Tarehe hiyo pia Oktoba 11, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Njombe Mji na Simba; Mtibwa na Tanzania Prisons; Lipuli na Majimaji wakati Stand United na Young Africans watacheza Oktoba 12, mwaka huu.

Novemba 15, 2017 Mbao itacheza na Young Africans; Kagera na Mbeya City; Stand United na Azam; Mwadui na Ruvu Shooting; Singida na Njombe Mji; Lipuli na Tanzania Prisons; Mtibwa Sugar na Majimaji wakati Novemba 16, Ndanda itacheza na Simba.

August 9, 2017

======
Jambo kubwa ni kuzorotesha ligi kwa mtu mmoja eti mchezo wa SIMBA VS AZAM umekhairishwa kisa Okwi kwenda kucheza mashindano kwenye timu yake ya taifa ndio maana kutoka kwetu bado ngumu kisoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi mchezo wetu ni siasa chafu, football tumesingiziwa!

Kwa Hisani Ya Watu Wa Mbeya!
 
Sasa hivi maamuzi ya TFF sharti yapate idhini Simba.
FIFA ina kanuni ipo very clear kuhusu idadi inayokubalika timu kuomba kuahirisha mechi iwapo wachezaji wake wapo kwenye majukumu ya National Team.
Haiwezi kuwa wachezaji wawili. Kama sijakosea ni watano! I stand to be corrected!
 
Kwani kuna kitu hakikushangazi nchini mwetu mkuu? Mbona hilo dogo sana halipaswi hata kukushangaza aisee
 
Kwa nini ligi ichezwe kipindi cha INTERNATIONAL games?! Pote ulaya & kwingineko ligi husimama kwa wiki mbili kupisha michezo hii.

TFF inapaswa kuiga mfano wa nchi zingine. Michezo yote isimame kupisha international games..!
 
Na hiyo ratiba ya International games watakuwa nayo kabla ya kupanga ratiba yao ya ligi. Nahisi wana justify vikao wapate posho
Kwa nini ligi ichezwe kipindi cha INTERNATIONAL games?! Pote ulaya & kwingineko ligi husimama kwa wiki mbili kupisha michezo hii.

TFF inapaswa kuiga mfano wa nchi zingine. Michezo yote isimame kupisha international games..!
 
Kumbuka tweet ya mtu aliyetarajiwa kuwa anajitambua. Halafu Kesho atateuliwa kuwa waziri wa michezo
 
Jambo kubwa ni kuzoroteaha ligi kwa mtu mmoja eti mchezo wa SIMBA VS AZAM umekhairishwa kisa okwi kwenda kucheza mashindano kwenye timu yake ya taifa dio maana kutoka kwetu bado ngumu kisoka

Sent using Jamii Forums mobile app
Ligi duniani kote zimesimama kupisha international games sasa hii ya okwi umeitoa wapi?
 
Ligi duniani kote zimesimama kupisha international games sasa hii ya okwi umeitoa wapi?
Ratiba iliyokuwepo inaonyesha Jumatatu Simba vs Azam. Ya awali kabisa ilikuwa jana 2nd September!
 
Ratiba iliyokuwepo inaonyesha Jumatatu Simba vs Azam. Ya awali kabisa ilikuwa jana 2nd September!
Labda sijamuelewa mtoa mada inamaana mechi iliyoahirishwa tz ni moja tu?
 
Labda sijamuelewa mtoa mada inamaana mechi iliyoahirishwa tz ni moja tu?
Sasa inaelekea ni zote.
Lakini ni upumbavu wa TFF. Wana taarifa zote kuhusu internationals wa kila timu na implication kwenye ratiba. Very stupid people at Bodi ya Ligi
 
Jambo kubwa ni kuzoroteaha ligi kwa mtu mmoja eti mchezo wa SIMBA VS AZAM umekhairishwa kisa okwi kwenda kucheza mashindano kwenye timu yake ya taifa dio maana kutoka kwetu bado ngumu kisoka

Sent using Jamii Forums mobile app
Je mechi zote siku hyo zihairishwa au ni upande wa Simba tu.
Halafu Mi naona TFF Hawana utaratibu mzur kma lig zingine,wenzetu wamesitisha michezo kwe lig kupisha mechi za kimataifa.
 
Ili Emanuel Okwi ambaye yuko kwenye hatihati kuukosa mchezo huo huko misri awe amerudi

17 PHD these are results
Acha ujinga na unafiki mechi zote za ligi ambzo zlitakiwa kchezwa j5 wamesogez mbele ili warekebishe ratiba iendane na mechi za timu ya taifa
 
Jambo kubwa ni kuzoroteaha ligi kwa mtu mmoja eti mchezo wa SIMBA VS AZAM umekhairishwa kisa okwi kwenda kucheza mashindano kwenye timu yake ya taifa dio maana kutoka kwetu bado ngumu kisoka

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha uongo sio mchezo mmja n mchezo yote acha ushabik maandazi
 
Mimi nadhani wameona mapato ya takuwa kidogo maana ni katikati ya wiki watu wengi watakuwa kazini,hivyo basi Jmoo itakuwa njema tuuuuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha ujinga na unafiki mechi zote za ligi ambzo zlitakiwa kchezwa j5 wamesogez mbele ili warekebishe ratiba iendane na mechi za timu ya taifa
Ujinga upi sasa???, Samaki mkunje angali mbichi, unazani TFF Simba wajinga???, lazima waandae mapema mbeleko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…