Bodi ya Ligi yatoa tamko kuhusu sakata la mechi ya Simba na Yanga

Mkuu umeongea ukweli , ila siku ya mechi bendi ilikuwa inajipanga kupiga gwaride sijajua kiongoz gani alikuwa anatarajiwa
 
Hapa mamlaka husika ndo zenye makosa yanga walifata kanuni na simba wakafata maagizo baadae wakageukia kanuni ...

Sema ata simba wenyewe mapungufu ni mengi
 
Mkuu umeongea ukweli , ila siku ya mechi bendi ilikuwa inajipanga kupiga gwaride sijajua kiongoz gani alikuwa anatarajiwa
I see... hili sikulifahamu!
 
Reactions: Lee
Nasoma huku natamani kucheka kwa uchungu. Bodi ya league sisi tumeambiwa tu tumefwata amri ya TFF. TFF sisi tuliambiwa tu lakini tunasikitika sana. Pumbavu wakubwa hawa. Kuna watu wanataka kumsingizia Mama lakini na uhakika sio Mama ingekuwa Mama kawaomba hakuna ambaye angempinga wote wangekubali kwa heshima ila hapa kuna watu wamejificha nyuma ya pazia na Bodi ya league na TFF hawataki kusema ukweli. Bodi wamejitoa wao wamewatupia mzigo TFF. TFF bado wanaomboleza na kusikitika wakimaliza matanga watasema. Dawa ya hawa mbwa wakipanga mechi watu wasiende uwanjani mara hii washabiki wa team zote watizame kwenye TV tu wasiende ndio dawa ya hawa kwa nia nzuri tu na mstakabali wa mpira TZ ili ujinga wa namna hii usirudiwe kwa team zote na sheria zote.
 
Mbona kwa maelezo hayo inaonekana kama Yanga ndio anataka kutupiwa jumba bovu?
 
Wamekubali hata wasimamizi pia hawakuwepo kwaajili ya mchezo.. hawa wababaishaji tu, unaweza kukuta wasimamizi waliambiwa mechi saa 4:00 usiku.
 
mbona wanaelezea tukio ambalo wote tunalijua badala ya kutoa maamuzi????
 
Reactions: Lee
Pia taarifa ya Bodi inaonesha haikupata maelekezo kutoka serikalini. Huko serikalini nako, hawajui nani aliyetoa taarifa hiyo. Sasa jamii ya soka imshike shati nani kutokan na mauzauza yaliyotokea, yanayoshawishi kuwa watu wabukwa wapenzi wa timu fulani kati ya hizo mbili, wanaashiria kupanga njama hizo kwa masalahi wanayoyafahamu wao!
Heads must roll down this time arounds...the victims ;our soccer caretakers vested to over see the game!
 
Reactions: Lee
Mtuhumiwa kaanza kujieleza hadharani. Wanatakiwa wajiudhuru. Eti timu hazikukaguliwa, kama hazikugaliwa nani aliwaambia waamuzi wasikague? Mtatajana tu.
Mkuu, hii kitu imechezwa na TFF sasa baada ya kuona maji yamewafika shingoni wamekumbuka kumbe ni bodi ya ligi ndo jukumu lake hivo TFF wanataka kujikosha kwa kupeleka tatizo kwenye bodi ya ligi. Nawashukuru kwa kuuruka mtego huo. TFF walisema wamepokea maagizo toka wizarani lakini mpaka sasa wizara husika ipo kimya tu. FIFA hiyo inakuja muda si mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…