Bodi ya Maslahi na Mishahara katika Utumishi wa Umma irejeshwe

Bodi ya Maslahi na Mishahara katika Utumishi wa Umma irejeshwe

dndagula

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
1,602
Reaction score
1,650
Rais Samia aliwahi kuelekeza mamlaka zinazohusika kurejesha Bodi ya Mishahara na maslahi katika utumishi wa umma iliyoanzishwa na Rais wa awamu ya nne na kisha kuvunjwa kipindi cha awamu ya tano.

Kutokuwepo kwa bodi hii hadi sasa na kuhamishia masuala ya maslahi idara kuu ya utumishi imeleta mgongano wa kimajukumu na kimaslahi.

Jukumu la kushughulikia maslahi ni zito linahitaji chombo maalum kinachoangazia jukumu hilo pekee na kufuatilia tija na mwenendo wa uchumi kwa kufanya tafiti.

Nchi zilizoko SADC na EAC nyingi zina chombo hiki ila sisi tulikiondoa kwa kisingizio cha duplication of functions.

Nadhani ni muhimu kuangalia upya namna ya kuirejesha Bodi hii hata kama itaitwa Tume ya Mishahara kam nchi nyingine.

Rais alikwishaelekeza kifufuliwe kwa busara zake. Itekelezwe.
 
Kweli kila Mtu ale kwa urefu wa kamba yake.

Lengo lenu hususani ni kurudi zile zama za kujikadiria mishahara minono kwa kulamba zaidi ya M 40 kwa mwezi?

Kweli Bongo bahati mbaya, ni heri niende Ulaya.
 
Rais Samia aliwahi kuelekeza mamlaka zinazohusika kurejesha Bodi ya Mishahara na maslahi katika utumishi wa umma iliyoanzishwa na Rais wa awamu ya nne na kisha kuvunjwa kipindi cha awamu ya tano.

Kutokuwepo kwa bodi hii hadi sasa na kuhamishia masuala ya maslahi idara kuu ya utumishi imeleta mgongano wa kimajukumu na kimaslahi.

Jukumu la kushughulikia maslahi ni zito linahitaji chombo maalum kinachoangazia jukumu hilo pekee na kufuatilia tija na mwenendo wa uchumi kwa kufanya tafiti.

Nchi zilizoko SADC na EAC nyingi zina chombo hiki ila sisi tulikiondoa kwa kisingizio cha duplication of functions.

Nadhani ni muhimu kuangalia upya namna ya kuirejesha Bodi hii hata kama itaitwa Tume ya Mishahara kam nchi nyingine.

Rais alikwishaelekeza kifufuliwe kwa busara zake. Itekelezwe.
kweli aiseee hata hivyo ngoja tusubili mei mosi itakuwaje maana story ni nyingi sana makazini humu
 
Ninarudia tena wito wetu wa kupatiwa Tume ya Mishahara na Maslahi ambayo imevunjwa mwaka mmoja uliopita. Bodi hii irejeshewe kama zawadi kwenye mei mosi. Hili ni jambo muhimu sana hata mkuu wa nchi aliliona akatoa maagizo lakini utekelezaji wake unasuasua.
 
Umuhimu wake ulikuwa Ni Nini?
 
Watairudisha mara tu baada ya vita ya Urusi na Ukraine kuisha bila shaka.
 
Kufanya tafiti za mishahara na kuhuisha maslahi. Je hulijui hilo
Sidhani kama ilikuwa na nguvu. Nafikiri Kama ilivyo kwa mashirika ya umma, wanavyopeana pesa kulingana na makusanyo yao ya ndani.

Hata Watumishi walioko Halmashauri wangeweza kupunguziwa ugumu wa Maisha Kutokana na makusanyo ya ndani.

Halmashauri Kuna pesa nyingi tu lakini zinatumika kipuuzi tu.

Wanakopesha kisiasa vijana, Wanawake na walemavu wengine hawalipi. Na hizi ni pesa zisizo na riba, wakipewa Watumishi Maisha yao yatakuwa poa kabisa.

Leo, Wakuu wa Shule, Watendaji na Madiwani wanalipwa kwa pesa hizi, Halmashauri zinashindwa Nini kuboresha maslahi ya Mtumishi. Yaani mpaka ziagizwe?
 
Watu wa serikalini nyie wavivu sana. Hamstahili kulipwa chochote.
 
Mazingira ya utawala na utashi wa kisiasa wa uongozi awamu ya 5 ulifanya bodi hiyo idhitiwe sana kuhusu masuala ya mishahara na pengine maoni yake kupuuzwa.kwa awamu hii ya 6 inaweza kuwa na nguvu ninaamini hivyo
 
Akili zako zina matatizo. Wafanyakazi wa serikali wote ni wanaume? Acha ujinga binti.

IMG_2971zg.jpg
 
Uthibiti wa kila kitu haina afya kiuchumi. Siri ya mafanikio ya Mzee Mkapa ambao ndio pumzi ya uchumi wetu hadi sasa ni kuachana na tabia ya kuthibiti kila kitu.
Hadi maslahi ya watu mnataka kuthibiti? Wakati majukumu hayafanani hata kidogo.
 
Mojawapo ya changamoto za wazi zilizosababishwa na serikali ya awamu ya tano ni over control, over regulation. Controlling or regulating everything in the economy is as good as bad.
 
Back
Top Bottom