KERO Bodi ya mikopo acheni kutembelea ofisi za watu na kudai watu bila kuwa na uhakika

KERO Bodi ya mikopo acheni kutembelea ofisi za watu na kudai watu bila kuwa na uhakika

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Rutechula

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2024
Posts
392
Reaction score
347
Wanabodi, kuna tabia inayozidi kuonekana ambapo bodi ya mikopo inatembelea ofisi za watu ikiwa na orodha ya wadaiwa wa mikopo.

Cha kushangaza, orodha hii mara nyingi inajumuisha majina ya watu ambao hawajawahi kuomba mkopo wala kujua chochote kuhusu bodi ya mikopo, kwani walijilipia ada zao kikamilifu tangu mwanzo hadi mwisho wa masomo yao.


Kinachokera zaidi ni kwamba, ukijaribu kuwaomba ushahidi wa mkopo unaodaiwa, kama jina la benki, namba ya akaunti walikoweka mkopo huo, au nakala ya fomu uliyotumia kuomba mkopo, hawana ushahidi wowote. Badala yake, wanakutaka uwape au uwatajie Index Number ya cheti chako cha kidato cha nne.

Na ukifanya hivyo, mara nyingi hukuta kuwa huusiki kabisa na deni hilo. Baada ya hapo, utasikia wakisema, “Samahani, udaiwi.”

Ni muhimu kuwaomba bodi hii ifanye kazi kwa umakini zaidi. Wanapokwenda kudai mkopo, wahakikishe kuwa wana taarifa kamili na sahihi kuhusu wadaiwa badala ya kutegemea bahati nasibu.

Ni jambo linaloleta usumbufu mkubwa kwa watu wasiokuwa na uhusiano wowote na mikopo hiyo.

Hii ni bodi inayosheheni wasomi na wataalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA), hivyo inapaswa kuwa mfano wa usahihi na uwajibikaji.

Wanapaswa kuhakikisha kuwa kila hatua wanayochukua imezingatia ukweli wa taarifa walizonazo.

Kwa hiyo, tunasisitiza kwamba wanaodaiwa kweli walipe mikopo yao pamoja na faini wanazostahili. Lakini kwa wale wasiohusika, wasisumbuliwe bila sababu. Tafadhali bodi, simamieni kwa umakini zaidi hili suala
 
Bodi ya mkopo wababaishaji sana jamaa...tena sisi tuliosoma zamani kidogo ndiyo shida kabisa.
Wao wanachokijua ni kuwa kama ulisomea hapa Tanzania basi ulipewa mkopo kumbe siyo, ni ujinga tupu.
 
Hilo deni wanalonidai litalipwa na mwigulu Nchemba
 
Back
Top Bottom