Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu (HESLB) mbona tunaongezeana deni kila mwezi, shida nini?

Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu (HESLB) mbona tunaongezeana deni kila mwezi, shida nini?

nyangelekene

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2014
Posts
481
Reaction score
344
Sijaelewa shida nini ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu mwezi uliopita(wa kwanza) deni lilikua milioni 3 mwezi wa pili milioni 3, watu wengi wanalalamika madeni kuongezeka wengine wanamaliza lakini mwezi unaofuata wanakuta ongezeko tena. Shida ni nini?

Hakuna taarifa yoyote wala ufafanuzi au ndo urefu wa kamba yenu umefika hadi huko?? Hivi hamjui jinsi tumesota adi kulifikisha ilo deni mwisho?? Nini kiko nyuma ya ili deni lenu?

Mnaumiza watu sana, kwani hiyo rentation fee iliyotolewa na RAIS imeondolewa au ni geresha tu?? Au kuna deni lingine tofauti na mloweka kwenye salary slip?

Semeni shida ni nini kila mwezi deni la kwenye salary slip linapanda tu na watu wakija ofisini majibu yenu hayaeleweki 'damnt'.
 
Inaumiza sana. Hafu hawajali hata kutoa taarifa. Mimi liliisha ila wameanza kukata upya. Nawaibukia soon nitalala kwao.
 
Mi mwenyewe nimeangalia salary slip ya mwezi wa pili nimekuta limeongezeka badala ya kupungua, na hakuna ufafanuzi wowote ambao bodi wametoa
 
Naombeni email ya kuwasiliana nao niko chimbo huku ili nami nitoe langu
 
Bodi ya Mikopo ni kero kubwa Sana, uongozi wa pale inatakiwa ubadilishwe kuna Majambazi, Wahuni, wezi wako pale wanashirikiana na watu wa Hazina kupiga Hela za watu.

Lakini kuna siku hizo hela zitawatokea puani, Watu wengi wamemaliza Marejesho lakini kwenye salary slip bado yanakata, cha ajabu Mwezi January wamerekibisha watu wa Hazina na kupunguza deni kutokana na retention fees upumbavu uliofanyika Mwezi huu February ni ajabu kabisa wameongeza deni, tena Baya zaidi wakabadilisha na salary slip ya January.

Hili Mama Samia simamia haya Majambazi yaondoe, Haiwezekani Bodi na Hazina wasipeane Taarifa na mtu akapata haki yake.
 
Bob Balance ni zero lakini Hawa jamaa wanazidi kukata
Kwani wanashindwa kupeleka Marejesho yaliyokamilishwa Hazina, Kama waliweza kupeleka MakatO
Yaani hizi Mamlaka Hazina wadilifu kabisa ni Majizi tu
Dahh.. sasa mbona sio poa.
 
Embu Rais afanye namna tafadhali.

Sioni tofauti kwa salary slip...ila nikecheki online nimekuta pungufu tofauti na salary. Sasa sijui ni hazina ndo wanazingua au lah!

Inakera hii.
 
Back
Top Bottom