Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu (HESLB) wanatokaje awamu hii?

Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu (HESLB) wanatokaje awamu hii?

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Awamu ya tano ilikuwa na maupendeleo kibao. Mikopo ikawa inatolewa kwa watoto wanaosemwa ni wa walalahoi. Watoto wa tabaka la wafanyakazi - hata wale ambao mishahara yao ni kiduchu na haijapandishwa kwa miaka sita mpaka sasa, watoto wao wakanyimwa kukopa. Vigezo vya kutoa mikopo vikaangalia uwezo wa wazazi badala ya uhitaji wa watoto.

Watoto wa Tabaka la wanaosadikika wazazi wao hawana uwezo ndiyo limekuwa tabaka tambaji huko mavyuoni kwani wao mikopo ni asilimia 100 na hakuna longo longo la kubaniwa. Watoto wa Tabaka ambalo linasemekana wanazo watoto wao wamekuwa wakisoma kwa shida mavyuoni - maombi yao ya mikopo yanatupwa kuleeeee! Wanahangaika mnooo hawa watu - kisa tu inaaminika eti wazazi wao wana uwezo.

Bodi ya Mikopo hiyo kwa sasa inaendelea na uchambuzi wa maombi husika kukiwa na utofauti wa awamu ya tano na awamu hii. Awamu ya tano ilionesha kuwachukia wanaoonekana ni tabaka la walionazo hadi kudiriki kuwatambia kuwa wanafaa waishi kama "Mashetani" na tabaka la wasionazo waishi kama "Malaika" - na pengine ikawa hivyo kama ulivyo utaratibu wa utoaji mikopo kwa watoto wetu- Watoto wanaosemekana ni wa tabaka la chini wanaishi kama "malaika" na wale wa tabaka ambao wanaaminiwa eti wanazo watoto wao wanaishi kama "mashetani".

Kazi ipo kweli kweli - tunasubiri majina tuone kama matabaka haya yanaendelea! Badru na Nyahende ni wale wale wa Mwendazake au wamebailika na kuwa wa "Mama"?
 
Back
Top Bottom