Up-coming Teacher
New Member
- Jan 19, 2013
- 2
- 0
Bodi ya mkopo ya Elimu ya juu (HESLB) IMEGOMA/IMESHINDWA/IMEKATAA kutulipia ada (Tuition fees) ya mwaka wa masomo wa 2012/2013 . Sakata hili lilianza pindi ambapo mwaka huu wa masomo ulipoanza kwa baadhi ya Wanachuo wa SAUT-MWANZA kwa idadi inayopungua 210 kutokuyaona majina yetu kwenye karatasi za kusaini hela kwa mwaka huu wa masomo.
Baada ya kukosekana kwa majina yetu ambayo ndio hudhihirisha upatikanaji wa hela kwa wanafunzi ambazo ni za chakula na malazi (Meals and accomodation) ilipelekea kusota kwa muda wa miezi sita (6 months) kuishi bila ya kupewa hata shillingi na bodi kitu kilichopelekea baadhi ya wanachuo kuahirisha mwaka kutokana na maisha magumu ya chuoni hapo.
Kutokana na juhudi zetu binafsi mpaka kufikia hatua ya kwenda Bodi ya mikopo (Dar es salaam) baada ya kuona hatua zote za kutuma wajumbe zimeshindwa na hivyo kwenda wote kwa pamoja ndio suala hili likatatuliwa kwa ndani ya siku tano tu na kupewa hela zote tulizostahili kupewa. Pia fedha za special faculty na za research ka mwaka wa 3 na 4 zikatolewa na kubakia ada ambayo hupewa chuo moja kwa moja.
Kitu kinachosikitisha ni kuwa tokea tupewe fedha hizo kwa zaidi ya miezi sita iliyopita Bodi ya mikopo imeshindwa kutulipia Ada ikapelekea kuzuiwa kufanya mitihani ya mwisho ya semista ya pili ambapo badae Chuo kilituruhusu kufanya mitihani hiyo. Pamoja na juhudi za Chuo kuturuhusu kufanya mitihani kwa mategemeo ya Bodi kutoa fedha hizo hatima yake imepelekea matokeo ya wanachuo tunaodaiwa kuzuiliwa kitu ambacho kitasababisha kutokupewa tena fedha na Bodi kutokana na Bodi yenyewe kuhitaji matokeo ya wanachuo ili kuendelea kutoa fedha hizo.
Tatizo hili la kutokupewa hela hizi lilitukumba hasa wanafunzi wa mwaka wa pili, tatu na nne. Katika kufuatilia tatizo hilo mpaka linapata nusu ufumbuzi hakuna sababu iliyotolewa na bodi kuonesha kuwa nini chanzo cha tatizo hilo.
Kinachoendelea kutuweka katika sintofahamu hiyo ya Bodi kutokutulipia Ada ni pale ambapo fedha za masomo kwa vitendo (Field) kwa wanafunzi wa idara ya elimu tuliokumbwa na tatizo hilo kupewa mwishoni mwa mwezi wa saba bila gogoro. Sasa tunaomba kuuliza tatizo ni nini mpaka kutokulipwa kwa Ada hiyo? Je, wanafunzi walio na tatizo hili wanaotarajia kuhitimu mwaka huu watasaidiwa vipi kulipa Ada hiyo? Je, ni maleengo ya Bodi kupunguza idadi ya wasomi nchini? Kuna nini nyuma ya pazia ya hela hizo za Ada ya watoto wa masikini? Je, ni muendelezo wa Ufisadi ndani ya Bodi ya mikopo? Wenye mamlaka juu katika nchi hii hasa Wizara ya Elimu na idara zinazohusika na tatizo hili tunahitaji msaada wenu.
WANAFUNZI WENYE TATIZO
SAUT-MWANZA