Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu mnakwama wapi?

Subiri salary ya mwezi wa saba itoke uangalie badiliko kama halieleweki funga safari uje Buguruni Tazara bora upoteze laki 2 uokoe milioni 3
 
Mimi nimeanza kulipa tangu 2016 mwishon lakin nimeomba statement online at bado nadaiwa 3.6m na nilikopeshwa 9m na nimeishawalipa 6.5m vrf pamoja na penalty ilikuwa 6m
Nakushauri fika ofisini kwao
 
Mkuu unawezaje kuangalia deni lako bila kufika ofisini loan board
Hilo sawa deni unaliona na control NBA unaiona haya sema uwalipe Sasa unadaiwa laki tano ila unaona deni milion kumi unasema ngoja niwatafute tuweke sawa hili tatizo hapo ndio shida huja wanakuomba details zako baada ya hapo sm hawapokei na namba yako wanaipiga black list
 
Huu uzi mzuri sana miye nawaomba wahudumu Kanda ya ziwa mwanza nipeni statement yangu mmekuwa kipere sm hapokei ila Kila mlichotaka nimewapa jina ni hili hili angalieni mezani kwenu Kuna makaratasi yangu
Funny....
 
Hao HESLB ni watu wa Hovyohovyo sana.

Utafikiri waliopo kwenye hizo ofisi hawana elimu au hawafahamu kabisa matumizi ya TEHAMA.

Kamwe hawajibu Email
Kamwe hawajibu SMS
Kamwe hawapokei simu

Sasa sijui waliweka zile namba za mawasiliano na emails zanini

Tangu miaka ya nyuma nikafikiri watabadilika kumbe ni walewale na uzembe wao.
 

Niwaulze waliopata statement tayar ile value retention fee before 1 May 2021 wameiwekaje?na kumbuka ilifutwa kabisa lakin wenyewe wamekaidi kuiondosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…