Bodi ya mikopo elimu ya juu mnatupeleka wapi!

mpolipoli

New Member
Joined
Mar 28, 2013
Posts
1
Reaction score
1
Wanajamvi naomba mnisaidie kuikumbusha bodi ya mikopo elimu ya juu (HESLB) kutimiza wajibu wake ipasavyo kwa wateja wake(wanafunzi) ambao kihalali iliwaidhinisha kupata mikopo kwa wakati.

Nikiwa mmojawapo wa wanafunzi waliofanikiwa kuidhinishwa na bodi ya mikopo elimu ya juu kupata mkopo wa ada na chakula kwa mwaka wa masomo 2012/2013 nasikitika na inanipa wakati mgumu kuelewa hii bodi ina nia gani na sisi wanafunzi tuliopewa uhamisho na tume ya elimu ya juu(TCU).

Tangu mwaka jana mwezi wa kumi tulianza kufatilia juu ya kuhamisha mikopo hiyo ili itufikie kule ambapo TCU wametupangia kwa mara ya pili bila mafanikio.Mwanzoni tuliambiwa tusubiri mpaka returns kutoka vyuo tulivyopangiwa mara ya kwanza ambapo ingechukua takribani miezi 2.Lakini cha kushangaza hadi mwezi December-2012 bado hatukupata mikopo hiyo yaani ada na pesa ya kujikimu.

Kila tunapojaribu kuulizia majibu ni kwamba tatizo linashughulikiwa na ahadi za kisiasa.Mpaka sasa semister ya pili imeanza pesa hizo hatujapata,cha kujiuliza pesa hizo zimeenda awpi wakati mwanzo mlidai zipo vyuo tulivyopangiwa mwanzo,je za robo ya pili na ya tatu nazo mmepeleka vyuoni au ndio mmeingiza kwenye fixed account zenu wakati watoto wa walala hoi hamjui tunaishi vipi vyuoni.

Naomba muwe na huruma japo kidogo na muondoe majibu ya kisiasa mnatuumiza kwa kweli,hamjui tunakula nini na wenye nyumba wanatufukuza kwenye nyumba zao,tulipeni tusome tuikomboe nchi yetu.
 
bodi hii imejaa watu wenye roho mbaya na wasiojali umaskini wa mtanzania hawana utu wala huruma wanajifanyia kazi wanavyotaka na ile maana ya means test wameacha sasa wanasema aina ya kozi!
 
Na wale waliokata rufaa kimya mpaka sasa. Hii bodi ya mikopo ni janga jingine kwa mlalahoi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…