KERO Bodi ya Mikopo (HESLB) inatuzungusha kutupa refund tuliolipa madeni tukazidisha kiwango tangu Mwaka 2021

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni Mtumishi wa Serikali, nilikuwa mnufaika wa mikopo ya Bodi ya Mikopo (HESLB) wakati nikisoma Chuo Kikuu!

Baada ya kuhitimu na kufanikiwa kupata kazi, nikaamua kulipa mkopo wote niliokuwa nadaiwa na Bodi ili nifute deni kisha nikaomba kiasi ninachodaiwa.

Kilichotokea wakanipa balance inayoonyesha kiasi cha fedha walichokiandika lakini ikagundulika wamekosea kuniandikia deni, maana walizidisha fedha zaidi, changamoto hiyo haikuwa kwangu pekee, kuna wengine kadhaa ninaowafahamu pia walipata changamoto hiyo.

Tukawasiliana HESLB wakasema watafanya REFUND, kwa maana ya kurejesha kile kiasi ambacho kilizidi, hiyo ilikuwa Mwaka 2021.

Tulipoendelea kuulizia wakasema wapo kwenye mjadala wa kuhusu watakavyorejesha fedha hizo, lakini hadi sasa Julai 2024 hatujui Refund zetu zitalipwa lini.

Awali tulimua kuwa na subira kwa kuwa ni taasisi ya Serikali ambapo ndipo tulipo sisi lakini siku zinazidi kwenda, hakuna majibu na hatuoni dalili za kulipwa.

Kuna kipindi walisema tusubiri Siku 90, lakini ikawa kimya mpaka sasa.

Machi 2023 tuliowaulizia wakasema wanasubiri Bunge likae kupitisha na kutoa kibali hizo fedha zirudishwe, lakini sasa hilo Bunge sijui ni tofauti nah li tunalolijua sisi au linatarajiwa kukaa mwaka gani?
 
Chukulia tu kama pesa iliyopotea baada ya kupigwa roba na vibaka maisha mengine yaendelee!
 
Back
Top Bottom