Bodi ya Mikopo (HESLB) tunaomba kujua kuna ubaya gani retation fee kwa wadaiwa ikasemehewa?

scatter

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2013
Posts
1,667
Reaction score
926
Serikali yetu ni ya wanyonge na wanufaika wa hii mikopo ni watanzania masikini je hamuoni kuna ulazima wa kuisamehe au kurekebisha sheria ili kipengele cha retation fee kipunguzwe au kuondolewa kabisa kwa sababu kuna watu wengi wana nia ya kurejesha mikopo yao lakini wakisikia suala la deni kuongezeka kila baada ya muda na ajira zenyewe ni ngumu ndio wanakata tamaa kabisa.

Hebu jaribuni kuiga makampuni ya simu Luku Dawasco jinsi walivyoweza kuanzisha mifumo shirikishi ili watu wa weze kujua taarifa zao kw urahisi kufika maofisini kwenu sio inshu.

Haya madeni yanaweza kuwa ya maisha kwa mtanzania wa kawaidaili kuweza kuyamaliza na pia MSIKARIRI KUWA LAZIMA UWE KATIKA GOVERNMENT SYSTEM NDIO ULIPE HILO DENI.

................................

MADHARA YA RETATION FEE 6%

Kwa mfano.
Daktari ambae amesomeshwa na bodi, asilimia kubwa deni lao huwa kati ya mil 25 mpaka 30.

Basic salary yake ni 1.5 Mil
Makato ya mshahara wake ni kama ifuatavyo,

Helsb 225, 000 TSH
PAYE 295,090 TSH
NHIF 42,420 TSH
Pension. 80, 000

Total deduction 642, 510 TSH
take home yake ni 857,590 TSH —ana watoto na anasomesha!

-----------------------------

Kwa sheria ya bodi ya mikopo, huyu bwana kwa mwaka ataweza kulipa 2.7Mil (225,000X12)

Hivyo katika deni lake la 30Mil , atakuwa amepunguza deni lake hadi 27, 300,000TSH ikifika mwisho wa mwaka wa fedha.

Mtu huyu atapaswa kuanza mwaka wa fedha mpya akiwa na deni la 27, 300, 000 TSH.

Lakini sheria ya bodi inasema hapana, unatakiwa kuongezewa 6% ya 30 mil ambayo ni 1.8 Mil

Hivyo deni analopaswa kuanza nalo ni 27,300,000+ 1.8 Mil sawa na 29, 100, 000 TSH.

Kwa mwaka unaofuata tena, atafanikiwa kuipunguza hiyo 29,100,000 Mil hadi 26,400,000 Mil na ndiyo ni kianzio cha deni lake kwa mwaka mpya uliofuata.

Sheria ya bodi itasema hapana, hii 26,400,000 lazima iwekwe 6% ya 30Mil ambaye ni 1.8

Hivyo 26,400,000+ 1.8 mil

Deni jipya kwa mwaka mpya uliofuata itakuwa ni 28,200,000Mil badala ya 26,400,000 and the list goes on.

Yaani utakuwa unakwenda mbele na kurudi nyuma mpaka unastaafu.

Sheria ya mwaka 2016, inazidi kusema kuwa, ikiwa muhusika mpaka anastaafu, hajafanikiwa kumaliza deni lake, basi pension yake itafidiwa.

Yaani, Ikiwa una pension ya 15 Mil , na deni lako lilibaki 20 Mil , Bodi itakula zote 15 Mil na itakudai 5 Mil na hiyo 5 mil itazidi kuongezeka kadiri miaka inavyokwenda mbele, ni hatari sana na mbaya zaidi watumishi wengi hawajui hii sheria.

Ikitokea pension yako imeliwa yote na bodi,maana yake unazeeka ukiwa huna kitu.

I just can't figure it out , ni sheria kandamizi dhidi ya mtoto maskini iliyopitishwa na wabunge wetu tukufu.

Ni kwamba mtoto wa maskini hatoweza kumaliza hili deni , ni deni la maisha hasa waliosoma makozi ya sayansi kama udaktari, Nesi, famasi , na injinia na wale waliosoma nje ya nchi.hawa wote madeni yao si chini ya 25Mil or so. It is a detrimental to these poor people, and Unfair.

MAPENDEKEZO
1. Serikali ipitie upya hii sheria, na ifutilie mbali hiyo incremental ya 6% kwa kila mwaka, it is not even practical, watu wengi wanakufa na hayo madeni tena bado yakiwa makubwa mno.

2. Irudishwe asilimia 8% au 10% badala ya 15% ya makato ya bodi, kwa sababu watumishi wa umma ndiyo wanufaika na hii mikopo, na wengi wanaangamia hali zao malikiti sokoni.

3. Bodi ya Mikopo itoe elimu maredioni juu ya utaratibu wa urejeshwaji wa haya makato WaTZ wengi haijui kitu kuhusu mambo ya sheria.

4. Sheria ya kuchukua pension ya watumishi walioitumikia serikali hadi kustaafu itolewe kwa Sababu ni mateso makubwa yatakuwa kwa hawa watu na hii ni jamii yetu inayoitumikia serikali ya Jamhuri miaka nenda rudi.

Watumishi wa umma wengi wanastaafu wakiwa maskini na fukara, uwachukulie tena hizo pesa za pension, kweli ? Doh tutapata laana katika nchi.

USHAURI
1. Kwa wazazi ambao wanajiweza, achaneni na mambo ya kuwasukumizia watoto wenu kwenye mikopo mpaka muelewe vyema sheria ya marekebisho, hiki ni kilema cha maisha kwa wale ambao deni lao ni above 20Mil.

2. Pia wahusika hakikisheni mnaipitia hii sheria na muelewe marejesho yake, you need to take precaution. Kama huelewi mtafute Mwanasheria akuelewesheni ni hatari sana fuatilieni haya mambo.
 
Kama waliweka makato ya 15% bila kujalisha moja ya tatu ya mshahara hicho unacho omba unadhani watakizingatia kwa sasa? Labda siku za usoni
 
Kama waliweka makato ya 15% bila kujalisha moja ya tatu ya mshahara hicho unacho omba unadhani watakizingatia kwa sasa? Labda siku za uso
Bila kupepesa macho walikosea na pia ni muda sasa wabadilike na madeni yote yawe katika platform za kidigital
 
BODI YA MIKOPO NA SHERIA MPYA NI UPATU KWA MWAMVULI WA SERIKALI

Bodi ya Mikopo imewanufaisha watanzania wengi sana ikiwa ni pamoja na kuwajengea watanzania misingi ya kielimu kwa ajili ya future katika maisha yao. Aidha, Asilimia 80 ya wanufaika wa mikopo ya bodi ni wale kina KAYUMBA Yaani watoto wa maskini.

Sheria ya mwaka 2016 ya bodi ya mikopo iliyofanyiwa marekebisho ni sheria ANGAMIZI kwa watoto maskini.

Sheria imeweka wazi ( Watz wengi hawana tabia ya kujisomea) kuwa marejesho ya mkopo yatakuwa ni kwa 15%, na deni hilo litakuwa linaongezeka kila mwaka wa fedha kwa asilimia 6% ya deni halisi la mwanzo.

Kwa mfano:
Daktari ambae amesomeshwa na bodi, asilimia kubwa deni lao huwa kati ya mil 25 mpaka 30.

Basic salary yake ni 1.5 Mil
Makato ya mshahara wake ni kama ifuatavyo,

Helsb 225, 000 TSH
PAYE 295,090 TSH
NHIF 42,420 TSH
Pension. 80, 000

Total deduction 642, 510 TSH
take home yake ni 857,590 TSH —ana watoto na anasomesha!

-----------------------------

Kwa sheria ya bodi ya mikopo, huyu bwana kwa mwaka ataweza kulipa 2.7Mil ( 225,000X12)

Hivyo katika deni lake la 30Mil , atakuwa amepunguza deni lake hadi 27, 300,000TSH ikifika mwisho wa mwaka wa fedha.

Mtu huyu atapaswa kuanza mwaka wa fedha mpya akiwa na deni la 27, 300, 000 TSH.

Lakini sheria ya bodi inasema hapana, unatakiwa kuongezewa 6% ya 30 mil ambayo ni 1.8 Mil

Hivyo deni analopaswa kuanza nalo ni 27,300,000+ 1.8 Mil sawa na 29, 100, 000 TSH.

Kwa mwaka unaofuata tena, atafanikiwa kuipunguza hiyo 29,100,000 Mil hadi 26,400,000 Mil na ndiyo ni kianzio cha deni lake kwa mwaka mpya uliofuata.

Sheria ya bodi itasema hapana, hii 26,400,000 lazima iwekwe 6% ya 30Mil ambaye ni 1.8

Hivyo 26,400,000+ 1.8 mil

Deni jipya kwa mwaka mpya uliofuata itakuwa ni 28,200,000Mil badala ya 26,400,000 and the list goes on.

Yaani utakuwa unakwenda mbele na kurudi nyuma mpaka unastaafu.

Sheria ya mwaka 2016, inazidi kusema kuwa, ikiwa muhusika mpaka anastaafu, hajafanikiwa kumaliza deni lake, basi pension yake itafidiwa.

Yaani, Ikiwa una pension ya 15 Mil , na deni lako lilibaki 20 Mil , Bodi itakula zote 15 Mil na itakudai 5 Mil na hiyo 5 mil itazidi kuongezeka kadiri miaka inavyokwenda mbele, ni hatari sana na mbaya zaidi watumishi wengi hawajui hii sheria.

Ikitokea pension yako imeliwa yote na bodi,maana yake unazeeka ukiwa huna kitu.

I just can't figure it out , ni sheria kandamizi dhidi ya mtoto maskini iliyopitishwa na wabunge wetu tukufu.

Ni kwamba mtoto wa maskini hatoweza kumaliza hili deni , ni deni la maisha hasa waliosoma makozi ya sayansi kama udaktari, Nesi, famasi , na injinia na wale waliosoma nje ya nchi.hawa wote madeni yao si chini ya 25Mil or so. It is a detrimental to these poor people, and Unfair.

MAPENDEKEZO
1. Serikali ipitie upya hii sheria, na ifutilie mbali hiyo incremental ya 6% kwa kila mwaka, it is not even practical, watu wengi wanakufa na hayo madeni tena bado yakiwa makubwa mno.

2. Irudishwe asilimia 8% au 10% badala ya 15% ya makato ya bodi, kwa sababu watumishi wa umma ndiyo wanufaika na hii mikopo, na wengi wanaangamia hali zao malikiti sokoni.

3. Bodi ya Mikopo itoe elimu maredioni juu ya utaratibu wa urejeshwaji wa haya makato WaTZ wengi haijui kitu kuhusu mambo ya sheria.

4. Sheria ya kuchukua pension ya watumishi walioitumikia serikali hadi kustaafu itolewe kwa Sababu ni mateso makubwa yatakuwa kwa hawa watu na hii ni jamii yetu inayoitumikia serikali ya Jamhuri miaka nenda rudi.

Watumishi wa umma wengi wanastaafu wakiwa maskini na fukara, uwachukulie tena hizo pesa za pension, kweli ? Doh tutapata laana katika nchi.

USHAURI
1. Kwa wazazi ambao wanajiweza, achaneni na mambo ya kuwasukumizia watoto wenu kwenye mikopo mpaka muelewe vyema sheria ya marekebisho, hiki ni kilema cha maisha kwa wale ambao deni lao ni above 20Mil.

2. Pia wahusika hakikisheni mnaipitia hii sheria na muelewe marejesho yake, you need to take precaution. Kama huelewi mtafute Mwanasheria akuelewesheni ni hatari sana fuatilieni haya mambo.

©️2021

IMG-20210110-WA0062.jpg
 
Magufuli kaharibu uchumi wa nchi kwa kiburi chake na sasa anatamani mishahara ya watumishi wote nchini.
Kaharibu vyanzo vikubwa vya taifa kupata pesa anatamani kutangaza watumishi wote wasilipwe ili ajenge nchi.
UZALENDO ANAHISI NI UMASIKINI.
 
Ndugu zangu mimi nimekuwa napambana sana na bodi ya mikopo.
Tatizo lao hawana taarifa sahihi kuhusu nani anadaiwa na anadaiwa kiasi gani...wameendelea kutegemea taarifa za kughushi kuwaumiza watanzania na madeni ya ajabu.

Kwa ufupi tutafute pesa ili watoto wetu tuwanusuru na hili zimi linaitwa bodi ya mikopo ndugu zangu.

Wahubirie watu wote mnaowafahamu....ikiwezekana wakope bank ama saccos wapate pesa wawalipie watoto wao lakini wasithubutu kuomba mkopo wa bodi ya mikopo....Nawasihi sana ndugu zangu
 
Da yani twafa bodi ambayo inaweka top up. Kwenye mkopo wa mteja. Huu ni uuaji.
 
Kama waliweka makato ya 15% bila kujalisha moja ya tatu ya mshahara hicho unacho omba unadhani watakizingatia kwa sasa? Labda siku za usoni
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2021-01-10 at 8.13.28 AM.jpeg
    WhatsApp Image 2021-01-10 at 8.13.28 AM.jpeg
    46.2 KB · Views: 4
Waziri wa Elimu aondoe Ratantion Fee.
Serikali iwasaidie watumishi wake waishi maisha marahisi.
 
Back
Top Bottom