Makosa wafanye wao kukata zaidi ya deni mnufaika unalodaiwa halafu ukiwafuata wanakupa statement wenyewe inaonyesha kweli umekatwa zaidi. Badala ya kuhakiki deni lako na kukuandika hundi wanakwambia rudi nyumbani na kajisajiri kwenye mfumo udai kurudishiwa makato yaliyozidi.
Wanakwambia subiri baada ya miezi 3 ndipo watapitia kuhakiki malipo yako. Ukiwapigia kuwakumbushia muda umepita simu anapokea afisa mmoja ana kiswahili cha kule ndege ilikotua majini. Anakushambulia kwa maswali kuwa ulieleweshwa usubiri muda gani, utadhani wewe ndiye mwenye makosa kukatwa zaidi ya deni halisi.
Wakati mwingine japo kuna mambo sikukubaliana na mwendazake inabidi nimkumbuke tu. Hivi mama yetu huwezi kuwaambia watulipe ndani ya siku 3 badala ya miezi 3. Hivi Prof Mkenda na hili nalo ukiwambia watulipe ndani ya siku 3 watakugomea mpaka tena uwashitaki kwa Spika?