Bodi ya Mikopo (HESLB) yasogeza mbele muda wa kuomba mikopo ya Chuo Mwaka 2024/25

Bodi ya Mikopo (HESLB) yasogeza mbele muda wa kuomba mikopo ya Chuo Mwaka 2024/25

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
IMG-20240831-WA0136(1).jpg

Wahitimu wa Diploma Chuo cha DIT hatujapata AVN Namba, tunashindwa kuomba Mkopo, tunaomba Bodi iongeze muda wa maombi

KUONGEZWA KWA MUDA WA MAOMBI YA MIKOPO 2024/2025

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwafahamisha Waombaji wa mikopo na Umma kwa ujumla kuwa muda wa kuwasilisha maombi ya mikopo umeongezwa mbele hadi tarehe 14 Septemba, 2024.

Hatua hii imechukuliwa ili kuwapa fursa wale ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kufanya maombi ya mikopo katika muda uliokuwa umepangwa.

Itakumbukwa kuwa, awali Bodi ilianza kupokea maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao tarehe 1 Juni, 2024 na mwisho wa kuwasilisha maombi ulipangwa kuwa tarehe 31 Agosti, 2024.

Kupitia tangazo hili, waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2024/2025 ambao hawajakamilisha maombi yao wanashauriwa kukamilisha na kuwasilisha maombi yao ya mikopo ndani ya muda ulioongezwa.

Bodi inapenda kusisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe 14 Septemba, 2024.

IMETOLEWA NA:
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Jumamosi, Agosti 31, 2024
 
Nashkuru Mungu nilisoma bila mkopo, sio kwa kupenda bali kwa kukosa mkopo, sasa hivi nina deni kwa wazazi la kuwalipa na riba juu. 🙏
 
Back
Top Bottom