Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema imeshapeleka Tsh Billioni 122.8 katika vyuo na taasisi za elimu 81 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi.
Imesema wanafunzi wanaostahili kupata mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 ni 132,119, fedha wanazopewa ni kwa ajili ya malazi, posho na ada na kufafanua kuwa fedha za malazi na posho ni za siku 60 kuanzia Juni Mosi hadi Julai 30, 2020.
Hatua hiyo imekuja baada ya Rais John Pombe Magufuli alitangaza kufungua vyuo kuanzia Juni 1 na aliwapa siku tisa za kujiandaa ili kusiwe na changamoto kwa wanafunzi na vyuo wakisharudi shuleni.
Rais ameruhusu wanafunzi wa vyuo na wanafunzi wa kidato cha sita kuendelea na masomo akisema kuwa ni watu wazima ambao wanaweza kujichunga dhidi ya #CoronaVirus.