Bodi ya Mikopo ni Moja ya Taasisi Zinazoibia Wananchi Kwa Ulaghai

Mshangai

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2008
Posts
468
Reaction score
1,086
Mwezi November Bodi ya mikopo pengine kwa kuona imeishiwa fedha za kulipana posho zao ikatunga habari kuwa wale wote ambao wamekosa mikopo ila wanadhani walistahili kukopeshwa na au wamepata nafasi ila hawana uwezo wa kujisomeaha elimu ya juu wanaweza ku appeal.
Moja ya masharti ya kuappeal ni kutuma kwa M pesa shs 5,000/ kwa bodi. Huku wakielewa kuwa kutokana na shida walizo nazo maelfu ya watoto wa masikini lazima watatuma tuu appeal.
Ni kweli maelfu ya watoto wa masikini walifanya hivyo na hapo ikawa imetoka. Hela imeliwa hakuna taarifa nyingine yeyote kutolewa wala hakuna aliyepewa. Jee huo si wizi wa mchana kweupe? Kama Taasisi ya serikali inaamua kuwaibia watu wake mchana kweupe na serikali husika inafumbia macho jambo hilo ndio kusema inahusika na hujuma hizo. Kweli nchi hii ni ya aina yake.
 
Duh, Mkuu umefanya research katika vyuo vipi? mbona hapa kwetu IFM wana zaidi ya 22 walioappeal wamepata, kama haitoshi DUCE kuna watu watano wamepata! Mimi ni victim wa kukosa mkopo hata kwa rufaa pia, bado nachelea kukubaliana na thread yako japo siipingi. Nadhani kuna kitu kipo ila usikate tamaa, cha msingi tuombe MUNGU atie wepesi ili tuendelee na masomo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…