Huwa najiuliza, kama Taifa tuna nini akilini mwetu?
Haiingii akilini kuwakopesha zaidi ya milioni 13 vijana, tena kutoka familia masikini, ili wasome vyuoni halafu tushindwe kuzirejesha hizo hela.
Huwa nawaza, wahusika wanashindwa nini kutengeneza mfumo bora wa elimu?
Mfano, kujenga VETA, football academy, scheme za umwagiliaji, lunch za mifugo, viwanda vidogo vidogo ili kuziba pengo la ukosefu wa ajira.
Fikiria, Tanzania tunauza nini huko nje? Hapana, hata pamba stick za kuchokonolea masikio ni Made in China wakati ni vitu vya skills ndogo ndogo.
Hayo mamilioni yanayotumika kuwakopesha watoto wa masikini wakasomee ualimu wa Kiswahili na History, hebu jenga VETA, academy, scheme za umwagiliaji, viwanda vidogo vidogo.
Tengeneza u busy kwa watu, wazalishe ili kesho tuuze nje kwa zaidi ya asilimia 80.
Miti ipo, mabonde kama Maragarasi yapo, masoko hasa Afrika yapo, hali ya hewa Tanzania inasapoti karibu kila zao.
HESLB, oneeni huruma pesa za walipa kodi. Mimi mnadai zaidi ya milioni 13, nisipoajiriwa hizo fedha sizani kama zitarudi.
Niseme tu, nilichokiona kwenye usaili wa walimu, loan board mnapoteza fedha nyingi sana na vijana hawana matumaini. Wengi tumetokea katika familia masikini – huo ndio uhalisia.
Mtasema tujiajiri, lakini niambieni, ni wafanyabiashara wangapi au ni wajasiriamali wangapi nchi hii wenye uwezo wa kupata 30,000 kama faida kwa siku? Wangapi??