Bodi ya mikopo-ujambazi uliozidi ufisadi!

Bodi ya mikopo-ujambazi uliozidi ufisadi!

Amoeba

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2009
Posts
3,288
Reaction score
791
Hii inaumiza sana,
Unapotuma pesa kwa M-PESA unapewa transaction ID na VODA, Hiyo transaction ID unaitumia ku-confirm malipo HESLB ili uweze kuprint form ya maombi ya mkopo: mbaya kuliko, ukiingiza hiyo transaction id unaambiwa "imeshatumiwa na mtu mwingine" ukipiga simu HESLB wanakwambia "utakuwa umeiba transaction ID ya mtu mwingine"!!!! Ukipiga simu voda wanakwambia wasiliana na HESLB!!!!

Kinachonifanya niseme huu ni wizi ni jinsi ilivyo rahisi kuona nani kalipa ngapi kwa mawasiliano kati ya VODA na HESLB! Namba zote za simu zimesajiliwa; ni rahisi sana kuangalia jina la mtu aliyefanya transaction; au kuconfirm kama imetokea error MPESA wakaasign transaction ID moja kwa watu wawili!!! kitu ambacho ni unlikely! Naongea hivi kwa uchungu sana tu kwa sababu imetokea kwa jamaa zangu wawili, siku nne sasa na hakuna dalili za ama kurejeshewa pesa zao au kuthibitishiwa malipo!!

Pale HESLB kuna wakina mama wana majibu ya nyodo sana, hawajali hawa wanafunzi ama wazazi wao wanapata vp hizo pesa, huu ni wizi wa kipumbavu kabisa ambao haufai kufumbiwa macho!!!

Najua ni wengi sana watakaolizwa kwa mtindo huu! wegine hawana sehemu hata ya kuongea, lakn mimi nasema kwa niaba yao-WIZI HUU UTAUMIZA WENGI:angry:!
NCHII HII ITAENDELEA KWELI KWA UFISADI WA NAMNA HII, INSANE:angry:
 
kuna watu hawatapata hiyo pesa ya mkono, wanatumia technologia ambayo hawaijui vizuri, haha sijui nicheke
 
kuna watu hawatapata hiyo pesa ya mkono, wanatumia technologia ambayo hawaijui vizuri, haha sijui nicheke

Tatizo la tech linaanzia kwa haohao HESLB! hao waliowekwa kusimamia hizo tech na hao waliowekwa kutoa huduma kwa mteja ni utata mtupu; kama siyo wezi pia basi uelewa wao wa sysytem wanazomtumia ni mdogo sana! Hii ni mbaya sana.
 
laziam watakuwa wamewekana na ndugu zao bila kuangalia ufanisi au wataalamu wenye ujuzi wa hawa mambo, najua hakuna complication hata kidogo kwenye hii njia waliyoianzisha lakini inabidi wawe makini na waifanye kwa uangalifu hakutakuwa na malalaiko yoyote
 
They are INCOMPETENT!
 
Mkuu hzo procedures huwekwa makusudi kwa ajiri ya kuwasurubu watoto wa masikini

pili watoto wao (wa mafisadi) hawaitaji kupanga foleni M-pesa ili kupata hayo mahitaji,wao uongea kwenye simu, na HESLB officers huweka mambo yote sawa kwa kuhaidiwa rushwa

tatu,wale wafanyakazi wengi wao ni waajiriwa wa wakubwa na si kwa niaba ya watanzania walalahoi,alafu ile ni kati ya ofisi nyingi zilzoamua kujibadiri na kuwa vijiwe/maskani za watu,wanaingia kazini saa 3 alafu saa6 haooo!,

Nadhani hapa cha kufanya sikioni maana tatizo siyo ofisi tatizo ni mfumo wote wa serikali (the whole system is rotten) hata tukisema HESLB ivunjwe bado haitasaidia ,watafanya kilekile cha kuvua gamba wakati nyoka anabaki ni yuleyule,cha msingi tumwombe Mungu atuwezeshe tupate katiba mpya ambamo every segment of our life shall be stipulated in there
 
Kazi mnayo mwaka huu..nafkiri hii ni strategy ya kupunguza waombaji mkopo.
 
Back
Top Bottom