bodi ya mikopo vyuo vikuu ifutwe tu.

bodi ya mikopo vyuo vikuu ifutwe tu.

LEVEL

Senior Member
Joined
Jul 4, 2013
Posts
195
Reaction score
51
waliopendekeza kuwepo kwa bodi ya mikopo vyuo vikuu walikua na nia nzuri sana kuwasaidia watanzania kupata elimu ya juu kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla. lakini kwa maoni yangu mimi sioni umhim wowote wakua na bodi hii kwa sababu upatikanaji wa mikopo kwanza umekua mgumu sana kutokana na kutokua ni vigezo vinavyo julikana kwa wanachuo kupata mkopo, ucheleweshwaji wa mikopo kwa wanafunzi wanao bahatika kupata mikopo na malalamiko mengine yanayo ihusu bodi hii.
hivyo nionavyo mimi ni bora serikali yetu ingepunguza ada za vyuo vikuu ili watu tujisomeshe wenyewe, kuliko kuishi kwa mikopo ambayo inatufanya tuishi maisha ya wasiwasi vyuoni.
 
Kiuhalisia si rahisi sana kupunguza ada za chuo kikuu na bado mtu akajisomesha, kwa pesa inayotoka wapi? Mimi sidhani kama ni jambo linalowezekana kwa sasa kila mtu anayestahili akapata mkopo. Lazima kuwa na vipaumbele fulani fulani ili malengo fulani yatimie. Mf. Walimu wa History (kwa idadi yao ni wengi sana) na walimu wa Sayansi wako wachache sana. Huwezi kutumia random sampling kupata beneficiaries, lazima kuwe na preferential qualifications for a special purpose. Kuvunja bodi itokane na sababu nyingine labda za uwajibikaji na makosa ya kiutumishi na rushwa labda. Lakini ucheleweshwaji ni jambo la kawaida sana kutokana na procedures za kutoka kwa hela. Kwa sisi watumishi wa Umma kupata mshahara wa mwezi tarehe hadi 5 ya mwezi unaofuatia ni jambo la kawaida lakini hatuwezi kusema hazina ivunjwe au wizara ya elimu wajiuzuru. Cha kuomba hapo ni sera zibadilike ili ziweze ku accomodate most sensitive cases first and then the rest should as well be streamlined in the same way. Nikirudi kwenye hoja yako kwamba "mimi sioni umhim wowote wakua na bodi hii kwa sababu upatikanaji wa mikopo kwanza umekua mgumu sana kutokana na kutokua ni vigezo vinavyo julikana kwa wanachuo kupata mkopo" Upatikanaji ukiwa mgumu suala si kuvunja bodi ni kurekebisha tatizo, maana hata watakaochaguliwa kubadili nafasi hawaji na hela zao pale, zote zinatoka hazina moja. Ila niungane na wewe kwenye hoja kwamba kuna vitu vinapaswa kurekebishwa pale bodi ili upatikanaji wa mkopo uwe na vigezo vya wazi zaidi. Sisi wanafunzi wa vyuo tulipokwenda Bungeni kushinikiza serikali kurekebisha sheria ya mkopo wakati mikopo inarudi tena tulifanikiwa kwa mahitaji ya wakati ule. Kama kuna mahitaji mapya ni kutumia utaratibu mzuri kushinikiza. Mbona sisi tulifanikiwa na mpaka sasa watu wanapata mkopo hata kama kuna changamoto. Tumieni njia nzuri kama wasomi kupeleka hoja zitakazobadilisha mambo na kufanya yawe mazuri zaidi. Kila la kheri.
 
Back
Top Bottom