Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi itazamwe kwa ukaribu

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi itazamwe kwa ukaribu

run CMD

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2015
Posts
3,185
Reaction score
3,909
Baada ya HESLB kufunga maombi na kutoa twakimu ni wazi bodi hii inakosa muelekeo katika vipaumbele vya kozi za kutoa mikopo.

Katika soko la ajira na kujiajiri ufundi wowote ungefaa kuwa kipaumbele katika utoaji wa mikopo.

Pili kinachotolewa mkopo ni kozi au Hali ya mwanafunzi.

Ukiangalia kwa jicho la ndani wao wanatoa kwa kozi na si Hali ya mwanafunzi na inasikitisha zaidi kuona kozi hizo si zile za kujiajiri au za ufundi mfano Environmental Science, Petroleum Engineering, Ualimu, n.k zipo kwenye kipaumbele kuliko Mechanical Engineering au Civil Engineering.

Ni Nani aliwapa utafiti huo.

Vijana wengi pia wanasoma vyuo vya kati kwanini bodi hii ikiwa Nia Yao ya dhati ni kupambana na muelekeo wa taaluma siku za usoni wasiwekeze kwa Vijana hasa mafundi na kozi zenye uwezo wa kujiajiri kuliko kuajiriwa.

Ukiangalia Vijana wa ngazi ya diploma waliopata mkopo hawafiki hata 6000 nchi Nzima Hawa ndio mafundi wengi na ajira zisizo rasmi nyingi kuliko degree.

Wanafunzi wote wa diploma Electrical, Electronics, Civil, Mechanical wamekosa wote.

Kuna Haja ya bodi hii kutazamwa upya kwa muelekeo wa taifa Zima na vipaumbele.

Cc. Bodi ya Mikopo (HESLB)
 
Kwa akili ya kawaida mikopo inatakiwa itolewe kwa watu wa vocational sio wengine hao
 
HESLB ije kujibu hizi tuhuma, haiwezekani ma injinia wakose mkopo.
 
Back
Top Bottom