ndupa
JF-Expert Member
- Jan 25, 2008
- 4,403
- 148
TUMEKUWA tukisisitiza mara kwa
mara kwamba muundo wa Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HELSB), una walakini mkubwa. Bila
kutafuna maneno, tumekuwa tukisema
kwamba bodi hiyo haiwezi kufanya
kazi zake kwa ufanisi kutokana na
kasoro za kisera na kimuundo ambazo
zimeifanya bodi hiyo kufanya kazi
kama idara ya Serikali.
Kama hiyo haitoshi, wizara husika
nayo imekuwa sehemu ya tatizo, kwani
nayo pia imeshindwa kuisimamia bodi
hiyo ili itekeleze sheria zilizopitishwa
na Bunge kuhusu mikopo ya
wanafunzi. Ni jambo la kufadhaisha
kuona viongozi wa wizara husika
wakiungana na HELSB kulalamika
badala ya kubuni mbinu za kutatua
matatizo yanayowasibu wanafunzi wa
elimu ya juu katika kupata mikopo.
Katika kuendeleza utamaduni huo wa
kulalamika, Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru
Kawambwa alisema juzi kuwa, wizara
yake inatatizwa na suala la wanafunzi
waliokopa fedha kupitia HELSB
kutorejesha fedha hizo ili wanafunzi
wengi zaidi waweze kufaidika na
mikopo hiyo.
Alisema hadi Septemba mwaka huu,
fedha zilizokusanywa ni Sh23.3 bilioni
kutoka kwa wanafunzi 48,235 tu na
kwamba kiwango hicho ni chini ya
asilimia 50 ya fedha zilizotakiwa
kurudishwa. Katika kuonyesha jinsi
wizara yake ilivyokata tamaa kuhusu
uwezekano wa mikopo hiyo
kurejeshwa, alisema wanafunzi hao
wasiporejesha mikopo hiyo
watafuatiliwa na wakala maalumu
aliyeajiriwa na HELSB kwa lengo la
kuwafuatilia ambao hawajarejesha
mikopo hiyo.
Kama tulivyosema hapo juu, kauli hiyo
inaonyesha bayana kwamba ni ya mtu
aliyekata tamaa. Huku akikiri kwamba
tatizo hilo limekuwa changamoto
kubwa kwa wizara yake, alisema
wanafunzi hao waliorejesha mikopo
ndiyo wamegundulika na kwamba
idadi kubwa zaidi bado haijagundulika
na haijulikani wako wapi na
wanafanya kazi gani.
Pamoja na kusema HELSB imeajiri
wakala maalumu wa kufuatilia ambao
hawajarejesha mikopo, Waziri
Kawambwa alisema ameiambia bodi
hiyo kwamba hatakuwa na uhusiano
mzuri na bodi hiyo kabla haijafanya
kazi ya kuhakikisha mikopo hiyo
inarejeshwa, hivyo kuitaka bodi hiyo
kufanya kazi usiku na mchana
kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa.
Tafsiri ya moja kwa moja ya kauli hiyo
ya Waziri ni kwamba kuna uzembe
mkubwa katika bodi hiyo ingawa inao
uwezo wa kuhakikisha mikopo hiyo
inarejeshwa. Jambo la kushangaza ni
kuona anapata kigugumizi kuifukuza
bodi hiyo na kuteua mpya itakayokuwa
na dhamira na uwezo wa kuhakikisha
mikopo hiyo inarejeshwa, tena katika
kipindi kifupi. Tatizo hapa ni
utamaduni wa kuleana na kulindana
na hakuna mwenye uchungu wa
kuhakikisha fedha hizo ambazo
zimetokana na kodi za wananchi
zinarejeshwa.
Tunapata wakati mgumu kuelewa jinsi
watu wanavyoweza kuchukua mikopo
halafu wakaingia mitini, licha ya
kusaini mikataba iliyotayarishwa na
wanasheria wasomi na kuwapo sheria
ya Bunge inayosimamia mikopo hiyo.
Hatutaki kuamini kwamba mikataba
hiyo ilitayarishwa na kusainiwa
kienyeji, kwa maana ya kutobainisha
anuani za makazi na wakopaji
kutokuwa na wadhamini ambao mali
zao (collateral) zinakamatwa na
kunadiwa pindi wadhaminiwa
wanapotoweka kusikojulikana kama
Waziri Kawambwa anavyodai.
Matatizo yote hayo yasingetokea kama
Bodi ingekuwa na watu wabunifu na
waadilifu. Tunaambiwa baadhi ya
wafanyakazi wake wamepelekwa
mahakamani kwa madai ya kuchota
mamilioni ya fedha za mikopo. Ushauri
wetu kwa Waziri Kawambwa ni
kuisafisha bodi hiyo na kuteua mpya
itakayoleta ufanisi. Vinginevyo fedha
hizo za wananchi zitakuwa
zimekwenda kwa mganga,
hazitarejeshwa ngo.
mara kwamba muundo wa Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HELSB), una walakini mkubwa. Bila
kutafuna maneno, tumekuwa tukisema
kwamba bodi hiyo haiwezi kufanya
kazi zake kwa ufanisi kutokana na
kasoro za kisera na kimuundo ambazo
zimeifanya bodi hiyo kufanya kazi
kama idara ya Serikali.
Kama hiyo haitoshi, wizara husika
nayo imekuwa sehemu ya tatizo, kwani
nayo pia imeshindwa kuisimamia bodi
hiyo ili itekeleze sheria zilizopitishwa
na Bunge kuhusu mikopo ya
wanafunzi. Ni jambo la kufadhaisha
kuona viongozi wa wizara husika
wakiungana na HELSB kulalamika
badala ya kubuni mbinu za kutatua
matatizo yanayowasibu wanafunzi wa
elimu ya juu katika kupata mikopo.
Katika kuendeleza utamaduni huo wa
kulalamika, Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru
Kawambwa alisema juzi kuwa, wizara
yake inatatizwa na suala la wanafunzi
waliokopa fedha kupitia HELSB
kutorejesha fedha hizo ili wanafunzi
wengi zaidi waweze kufaidika na
mikopo hiyo.
Alisema hadi Septemba mwaka huu,
fedha zilizokusanywa ni Sh23.3 bilioni
kutoka kwa wanafunzi 48,235 tu na
kwamba kiwango hicho ni chini ya
asilimia 50 ya fedha zilizotakiwa
kurudishwa. Katika kuonyesha jinsi
wizara yake ilivyokata tamaa kuhusu
uwezekano wa mikopo hiyo
kurejeshwa, alisema wanafunzi hao
wasiporejesha mikopo hiyo
watafuatiliwa na wakala maalumu
aliyeajiriwa na HELSB kwa lengo la
kuwafuatilia ambao hawajarejesha
mikopo hiyo.
Kama tulivyosema hapo juu, kauli hiyo
inaonyesha bayana kwamba ni ya mtu
aliyekata tamaa. Huku akikiri kwamba
tatizo hilo limekuwa changamoto
kubwa kwa wizara yake, alisema
wanafunzi hao waliorejesha mikopo
ndiyo wamegundulika na kwamba
idadi kubwa zaidi bado haijagundulika
na haijulikani wako wapi na
wanafanya kazi gani.
Pamoja na kusema HELSB imeajiri
wakala maalumu wa kufuatilia ambao
hawajarejesha mikopo, Waziri
Kawambwa alisema ameiambia bodi
hiyo kwamba hatakuwa na uhusiano
mzuri na bodi hiyo kabla haijafanya
kazi ya kuhakikisha mikopo hiyo
inarejeshwa, hivyo kuitaka bodi hiyo
kufanya kazi usiku na mchana
kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa.
Tafsiri ya moja kwa moja ya kauli hiyo
ya Waziri ni kwamba kuna uzembe
mkubwa katika bodi hiyo ingawa inao
uwezo wa kuhakikisha mikopo hiyo
inarejeshwa. Jambo la kushangaza ni
kuona anapata kigugumizi kuifukuza
bodi hiyo na kuteua mpya itakayokuwa
na dhamira na uwezo wa kuhakikisha
mikopo hiyo inarejeshwa, tena katika
kipindi kifupi. Tatizo hapa ni
utamaduni wa kuleana na kulindana
na hakuna mwenye uchungu wa
kuhakikisha fedha hizo ambazo
zimetokana na kodi za wananchi
zinarejeshwa.
Tunapata wakati mgumu kuelewa jinsi
watu wanavyoweza kuchukua mikopo
halafu wakaingia mitini, licha ya
kusaini mikataba iliyotayarishwa na
wanasheria wasomi na kuwapo sheria
ya Bunge inayosimamia mikopo hiyo.
Hatutaki kuamini kwamba mikataba
hiyo ilitayarishwa na kusainiwa
kienyeji, kwa maana ya kutobainisha
anuani za makazi na wakopaji
kutokuwa na wadhamini ambao mali
zao (collateral) zinakamatwa na
kunadiwa pindi wadhaminiwa
wanapotoweka kusikojulikana kama
Waziri Kawambwa anavyodai.
Matatizo yote hayo yasingetokea kama
Bodi ingekuwa na watu wabunifu na
waadilifu. Tunaambiwa baadhi ya
wafanyakazi wake wamepelekwa
mahakamani kwa madai ya kuchota
mamilioni ya fedha za mikopo. Ushauri
wetu kwa Waziri Kawambwa ni
kuisafisha bodi hiyo na kuteua mpya
itakayoleta ufanisi. Vinginevyo fedha
hizo za wananchi zitakuwa
zimekwenda kwa mganga,
hazitarejeshwa ngo.