Baraza la Wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo lakutana kwa kikao cha mwaka cha Utendaji Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. George Nyatega amewapongeza wafanyakazi wa shirika hilo kwa ufanisi mkubwa waliouonyesha mwaka wa masomo uliopita 2012/2013 ambao umewezesha utoaji mikopo ya wanafunzi kuwa wa kiwango cha juu.
Bw. Nyatega alitoa pongezi hizo pia ikiwa ni kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Bodi ya Wakurugenzi inayosimamia taasisi hiyo.
Licha ya pongezi hizo, Mkurugenzi Mtendaji aliwaasa wafanyakazi kuongeza ufanisi na kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano ili kuhakikisha shirika hilo linazidi kuwa na umahiri mkubwa katika shughuli za utoaji mikopo na urejeshwaji wa mikopo ya wanafunzi.
Baraza la Wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) limekutana mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kikao cha siku mbili kujadili taarifa za kiutendaji za taasisi hiyo kwa lengo la kuangalia mafanikio na changamoto wanazozikabili na kuweka mikakati ya kuongeza kuboresha utoaji wa mikopo ya wanafunzi.
Katika waka ujao wa masomo 2013/2014 utakaoanza Oktoba 2013, Bodi inatarajia kukopesha wanafunzi 98,025 nak ati ya hao, wanafunzi 35,649 ni wa mwaka wa kwanza.
(Source Baraza la Wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo lakutana kwa kikao cha mwaka cha Utendaji