Bodi ya utalii tanzania kuendelea kuutangaza mlima meru

Bodi ya utalii tanzania kuendelea kuutangaza mlima meru

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

BODI YA UTALII TANZANIA KUENDELEA KUUTANGAZA MLIMA MERU

Wizara ya Maliasili na Utalii kupita Bodi ya Utalii itaendelea kuutangaza Mlima Meru pamoja na Hifadhi ya Arusha, Hifadhi ya Misitu Ziwa Duluti na Maeneo ya Utalii wa Utamaduni katika vijiji vinavyozunguka Mlima Meru kama vivutio vya utalii katika Mkoa wa Arusha.

Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) alipokuwa akijibu swali la Mhe. Zaytun Seif Swai (Mb) ambaye alitaka kujua Bodi ya Utalii itautangaza lini Mlima Meru kama kivutio cha Utalii.

Aidha Naibu Waziri aliongeza kuwa katika kuhakikisha Mlima Meru unafahamika kwa wadau mbalimbali wa Utalii Duniani, Bodi ya Utalii Tanzania imekuwa ikiandaa ziara za mafunzo za mawakala wa Biashara ya Utalii kutembelea Mlima kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii mbalimbali vinavyopatikana maeneo hayo.

”Utangazaji wa vivutio hivyo huzingatia shughuli za utalii zinazoweza kufanyika katika kivutio husika. Mathalan, Bodi ya Utalii Tanzania imekuwa ikiutangaza Mlima Meru kama kivutio cha shughuli za upandaji Mlima ambapo watalii huhamasishwa kupanda Mlima huo kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro” Alisema Mhe. Kitandula

Aidha katika hatua nyingine Naibu Waziri alisema kuwa Bodi ya Utalii imekuwa ikiwahusisha wajasiriamali katika maonesho mbalimbali ya utalii wakiwemo wanawake wanaojihusisha na bidhaa za sanaa kutoka Mkoa wa Arusha.

Mhe. Kitandula alisema kuwa serikali imejipanga kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana nyanda za juu kusini ikiwemo maporomo ya Kalambo.
 

Attachments

  • GGXMuLLXsAAa2j2tyuhjnm.jpg
    GGXMuLLXsAAa2j2tyuhjnm.jpg
    131.4 KB · Views: 6
  • IMG-20231110-WA0061juiokl.jpg
    IMG-20231110-WA0061juiokl.jpg
    278.4 KB · Views: 8
Back
Top Bottom