Bodi ya utalii Tanzania yamuita staa wa bundesliga kufanya utalii nchini ili kuitangaza Vivutio vya utalii Nchini

Bodi ya utalii Tanzania yamuita staa wa bundesliga kufanya utalii nchini ili kuitangaza Vivutio vya utalii Nchini

Shigganza

Senior Member
Joined
May 24, 2018
Posts
160
Reaction score
412
Bodi ya utalii Tanzania(TBT) kwa kushirikiana kushirikiana na taasisi ya Magnet Youth Sports Organization inatarajia kumleta mshambuliaji wa kimataifa wa Denmark mwenye asili ya Tanzania ambaye hivi sasa anayechezea klabu ya RB Leipzig inayoshiriki ligi kuu ya ujerumani ' Bundesliga' YUSSUF POULSEN kwa ajili ya kuzuru Nchini kwa shughuli za kitalii.

Ujio wa POULSEN unafuatia ziara ya kitalii ya makocha Andreas Pach na Martin Hammel wa ujerumani ya kupanda mlima Kilimanjaro Februari 15 hadi 19 mwaka huu na vivutio vingine lengo likiwa ni kutangaza utalii.

Ziara ya POULSEN Nchini Tanzania inatarajiwa kuitangaza zaidi Tanzaniakatika suala la utalii, ikizingatiwa mwanasoka huyo anacheza katika ligi ya Ujerumani ambayo ni miongoni mwa ligi kuu bora kabisa Duniani yenye mashabiki lukuki kutoka kila pande ya Dunia. Aidha ujio wa mwanandiga huyo unafungua ukurasa mpya kwa wanasoka wengine kutoka ligi ya ujerumani kuja Nchini kwa shughuli za kitalii.

Bila kumung'unya maneno Serikali ya awamu ya tano iko serious na imejizatiti kuhakikisha sekta ya utalii inaliingizia taifa fedha nyingi za kigeni.
 
Mna mchezaji kama Samata ila mnashindwa kumtumia kwa mambo kama hayo! Mnasubiri kutumia watu wengine ile hali tuna mtu sahihi kufanya hivyo kwa sasa.
Wana Macho Ila hawaoni
Wana masikio Ila Hawasikii

Akili au Matope??
 
Mjomba naona una kaukabila kwa mbaliiiii..umesema yeye ni nusu mtanzania na mama yake mdanishi. Ungeishia hapa tayari tumekuelewa, hii biashara eti mdigo wa tanga inatoka wapi? Hivi wadigo wako mikoa mingapi Tanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana mkuu nowsasa kama unamalizia hasira zako za vyuma kukaza kupitia nilichokiandika.
 
Utaona ziara hiyo inayoratibiwa na TTB zoezi zima kuanzia promotion, marketing, mahojiano yake yote , posti ktk social media platforms yatafanyika kwa Lugha ya 'kimatumbi' wakati walengwa ni wale 'mabeberu' wazungumzao Kiingereza , Kijerumani na Kispaniola.

Maana hata matayarisho ya kumleta huyo staa tayari bodi inajigamba ktk Lugha ya Kiswahili badala ya hizo nilizotaja kama kweli wanania ya kuitangaza Tanzania kwa ulimwengu.
 
Sijakasirika hata kidogo. Mambo na tabia za ukabila sizipendi kabisaa. Nadhani umenielewa. Ila la vyuma kukaza siyo utani..vimekaza haswaa..

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi sio mkabila, nimekua nikiwaona marais wote tangu Mwalimu Nyerere. Nimemuongelea katika hali ya utanzania, kwamba Mama Mdenish na Baba ni Mdigo, that is the truth and that has nothing to do with tribal feelings.
 
Back
Top Bottom