Bodi ya wahandisi ina matatizo makubwa, wqnachelewesha kuchapisha vyeti kwa makusudi nadhani kwa sababu zao binafsi, sasa kama mhandisi tayari umeshaandikishwa ukaandika ripoti na bodi ikakaa na kikubaliwa na mwisho ukaapishwa, ni nini kinachelewesha kuchapisha vyeti?
Kwani kuna mchakato wowote tena? Unakuta unasubiri cheti hadi miezi 3 hadi 6, na ukiwapigia simu au kwenda pale kuchukua unaambiwa subiri viko kwenye mchakato wa kuchapishwa, ni mchakato gani huo?
Naomba kuwasilisha.