Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya kuzinduliwa Mwezi Septemba 2022, Bodi mpya ya wakurugenzi ya CPB iliahidi kuleta mabadiliko makubwa katika taasisi hiyo na kuboresha utolewaji wa huduma na biashara ya nafaka Nchini Tanzania.
Katika kufanikisha lengo hilo, Bodi imekuwa ikifanya mabadaliko mbalimbali ya ki utendaji na kimkakati hadi sasa, ambayo bado yanaendelea ikiwemo kubadili mfumo wa biashara na kuachana na biashara ya rejareja, kusitisha ofisi za bodi nchini DRC na South Sudan, kuandaa mpango mkakati mpya wa masoko, na kupunguza urasimu.
Mnamo tarehe 30 Desemba 2022, Kikao cha dharura cha bodi ya wakurugenzi chini ya Mwenyekiti wake ndugu Salum Awadh Hagan, ilikaa na kupitisha azimio la kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo.
Pamoja na hilo, bodi pia imewasimamisha mkurugenzi wa fedha na utawala, mkurugenzi wa biashara, na meneja wa kanda ya Mashariki, meneja wa kanda ya ziwa, na meneja wa kanda ya kaskazini.
Maamuzi haya yamefikiwa baada ya bodi kushirikiana na uongozi wa juu wa Wizara ya Kilimo kupata ushauri, mwongozo, na kusaidiana katika mchakato wa kubainisha tuhuma mbalimbali za badhilifu, matumizi mabaya ya ofisi, na kutoonyesha uwezo wa kuweza kuivusha bodi kwenda hatua ya mbele zaidi.
Bodi itaunda timu maalum kwa ajili ya kufanya uchunguzi zaidi kabla ya maamuzi mengine hayajatolewa.