George Betram
JF-Expert Member
- Oct 10, 2015
- 4,672
- 6,272
Nina tatizo hilo maisha yangu yote. Ila mimi nikioga mchana ndio nawashwa mwili mpaka nijifute nipake lotion na kuvaa nguo. Nikioga asubuhi au jioni baada ya mazoezi siwashwi hata nisipopaka lotion.Kaka hata mm nilishawahi kuwa na tatizo kama hilo.Kwa kweli mpaka leo duniani hakuna daktari anayejua tiba ya hilo tatizo sababu mm nilizunguka hospitali nyingi sana na kufanya vupimo vingi hakuna kilichoonekana tofauti.Nadhani mafaktari au fani ya utabibu hilo halimo kwenye sylabus zao.
cha kufanya unapooga usijifute na taulo kwa kujiburuza buruza ila jifute kama unajikanda kanda.Ukifanya hivyo hutawashwa kabisa.Mm hii solution nilipata kwenye blog moja hivi tena kwa shida mno.
Try that kisha unipe matokeo kwa kuni pm.
You nailed it!!Pengine una allergy.
1. Kuna kemikali katika maji haipatani na ngozi yako.
2. Kuna kemikali akatika sabuni haipatani na ngozi yako.
3. Maji ni aina gani? Ya bomba? Ya kisima?
"Hard water" yanaweza kukuwasha Kama yana calcium nyingi.
4. Oga maji ya vugu vugu au baridi. Kuoga kwa muda mwingi na maji ya moto inaondoa kinga ya ngozi ya mafuta ya ngozi na kukupa uwasho.
5. Usibadilishe sabuni au shampoo Mara kwa mara.
6. Tumia sabuni yenye povu dogo kama za watoto wadogo. Sabuni nyingi zinatengenezwa na nazi. Nazi ina kemikali Sodium lauryl sulfate, inakupa uwasho.
7. Sabuni unayotumia kufua foronya na taulo haipatani na ngozi yako.
8. Tumia cream baada ya kuoga.
9. Onana na daktari wa ngozi ili upimwe kama una allergy na kitu au chakula.
10. Kuna ugonjwa wa ngozi unaitwa Aquagenic Pruritus. Ngozi haipendi maji. Ukioga tu, unawashwa. Wanaweza kukupima kama unao.
Daktari wa ngozi atakupa skin test kujua kama una allergy na kitu gani au wanaweza kuchunguza kwenye damu pia.
cholinergic urticaria ni ugonjwa unaotokana na allergy na jasho lako mwenyewe. Huu pia unaweza kupimwa na daktari wa ngozi.
peleka maji maabara hasa kama ni ya kismani.
Kama ushauri wa Tokyo hapo juu ukiufanyia kazi naamini utaleta mrejesho mzuri!!
Lakini pia jizoeshe kutembelea saluni za kike ambazo wanafanya massaji! Ukifika omba mdada mzuri akufanyie body scrub angalau mara moja kwa kila mwezi! kuna scrub nafanyiwaga ya chumvi nakuhakikishia itatoa wadudu wote wanao washa kwenye huo mwili!!
nitajaribu hii kaka..!Kaka hata mm nilishawahi kuwa na tatizo kama hilo.Kwa kweli mpaka leo duniani hakuna daktari anayejua tiba ya hilo tatizo sababu mm nilizunguka hospitali nyingi sana na kufanya vupimo vingi hakuna kilichoonekana tofauti.Nadhani mafaktari au fani ya utabibu hilo halimo kwenye sylabus zao.
cha kufanya unapooga usijifute na taulo kwa kujiburuza buruza ila jifute kama unajikanda kanda.Ukifanya hivyo hutawashwa kabisa.Mm hii solution nilipata kwenye blog moja hivi tena kwa shida mno.
Try that kisha unipe matokeo kwa kuni pm.
we acha mkuu...Hilo tatizo linakera, linaweza kugeuza mvivu wa kuoga.
Nilikua na hilo tatizo sijui liliishaje labda kwa sababu siku hizi kila siku natumia maji ya moto peke yake.
Hehehe! Yaani mtu ukitoka bafuni ni full kujikunakuna kila kona, pole sana, i understand your pain.
ahahahahah...Kama ushauri wa Tokyo hapo juu ukiufanyia kazi naamini utaleta mrejesho mzuri!!
Lakini pia jizoeshe kutembelea saluni za kike ambazo wanafanya massaji! Ukifika omba mdada mzuri akufanyie body scrub angalau mara moja kwa kila mwezi! kuna scrub nafanyiwaga ya chumvi nakuhakikishia itatoa wadudu wote wanao washa kwenye huo mwili!!
ndugu yangu pia niligundua huu ugonjwa unazidi pale utakapokua kwenye eneo lenye vumbi..!Mimi pia nina tatizo km hilo lkn najitahidi kupunguza muwasho kwa kutojisugua sn wakati wa kuoga na kujifuta kwa kitambaa chepesi au kanga baada ya kuoga, pia kwa kusafisha bafu na chumba chako kabla ya kuoga maana muwasho huwa mkali zaidi endapo chumba au bafu lako litakuwa na uchafu hasa wa kinyesi cha panya na mijusi. Kwakweli tatizo hili ni gumu sn kulitatua maana nimezunguka hospital kibao lkn sijapata suluhisho!!! Nafikiri kunahitajika uchunguzi wa kina kwa wataalamu wetu kugundua chanzo cha cha ugonjwa huu maana unasumbua mno.