Boeing wanalazimishwa kuzirudisha na kuzifanyia ukaguzi ndege za 787 Dreamliner

Boeing wanalazimishwa kuzirudisha na kuzifanyia ukaguzi ndege za 787 Dreamliner

Jamiitrailer

Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
80
Reaction score
208
Habari wadau,

Wakati jana tumepokea ndege nyingine mpya ya ATC,Boeing 787 Dreamliner, mamlaka ya anga ya America,US FAA, wameitaka kampuni ya Boeing kuzirudisha (recall) ndege zote aina hiyo iliyotua jana Zanzibar ili zifanyiwe kwanza uchunguzi wa kina na marekebisho.

Amri hiyo imekuja kutokana na hitilafu ya kujitegua kwa autopilot na hivyo kuifanya ndege kushuka bila uongozi(control).

Tukio la namna hiyo limesharipotiwa katika ndege 5 za namna hiyo,huku tukio la karibuni kabisa likiwa la mwezi Juni mwaka huu.

Ni kwa nini serikali ya Tanzania isingewaambia watu wa Boeing kwamba watasubiri kwa muda kuichukua ndege waliyoilipia tayari hadi pale itakapofanyiwa ukaguzi na marekebisho ili kuendana na agizo la mamlaka ya anga ya Amerika?

Kwa hali ilivyo, je ,serikali itairudisha tena ndege hiyo assembly plant kule Amerika ili ikaguliwe na kurekebishwa au itaiingiza hiyo ndege katika mizunguko ya safari bila kuzingatia hatari/risk...,ambayo ndege hiyo inaweza kusababisha wakati wowote?

Habari hii ipo katika main stream media zote katika hizi siku 2 na sijui kwa nini wahusika wa masuala ya anga na serikali kwa ujumla upande wetu hawajishughulishi kuangalia nini kina trend maeneo mengine duniani katika sekta wanayohusika nayo. Hapa chini ,ni hiyo habari kama ilivyo katika NBC news.

 
Kila kitu serikali ya chama dola kongwe inachogusa lazima kiwe na mushkeli.

Tatizo wanaongozwa na ilani ya CCM bila kuzingatia utaalamu wa mipango, mikakati na aeronautical science katika mradi kama huu, wanasukumwa na matamko ya mwenyekiti wa CCM.
 
Naona shida ipo kwenye viti vya marubani, kiti kilisogea mbele bila taarifa kikapelekea mfumo wa autopilot kuwa disconnected kitendo kilichopelekea ndege kuanza ku dive.
 
Naona shida ipo kwenye viti vya marubani, kiti kilisogea mbele bila taarifa kikapelekea mfumo wa autopilot kuwa disconnected kitendo kilichopelekea ndege kuanza ku dive.
Lini ndege imedive?
 
Watu wanachojali ni kutengeneza mazingira kwamba wanaupiga mwingi ili mwakani wagombee.
 
Back
Top Bottom