Boeing yasimamisha utengenezaji wa 737 Max

Boeing yasimamisha utengenezaji wa 737 Max

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Kampuni inayotengeneza ndege ya Boeng imetangaza kusitisha uzalishaji wa ndege aina ya 737 Max kuanzia mwezi Januari mwaka ujao, pamoja na sababu nyingine ili kuweza kupata ridhaa ya kiusalama kutoka kwa mamlaka za udhibiti kwa lengo la kufanikisha kuirejesha tena aina hiyo ya ndege angani.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo ya Kimarekani sababu nyingine ni gharama za uzalishaji. Aina hiyo ya ndege imezuiwa kuruka kutokana na ajali mbili za Ethiopia na Indonesia ambazo zimegharimu maisha ya watu 346.

Kiwanda hicho chenye makao yake makuu mjini Chicago kimetaja kusitisha uzalishaji wa aina hiyo ya ndege kutazigharimu ajira za watu 12,000 katika viwanda vya Renton na Washington.
 
Walikurupuka kuzifwatua ili kushindana na mshindani wake Airbus!
 
Back
Top Bottom