Bofya hapa uboreshe Elimu Tanzania

BUMIJA

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
5,950
Reaction score
11,295
Matokeo yamekua mabaya,yamezunguzwa mengi,toa maoni yako kama mdau tuweze kuwasaidia wanafunzi na Tulikomboe Taifa,maoni yote yatapelekwa Wizarani kuboresha.
 
Matokeo yamekua mabaya,yamezunguzwa mengi,toa maoni yako kama mdau tuweze kuwasaidia wanafunzi na Tulikomboe Taifa,maoni yote yatapelekwa Wizarani kuboresha.
Wewe ni nani katika wizara ya elimu?
Wewe maoni yako ni yapi kwanza katika kuboresha?
Kwanini umeficha id yako ?
Tutakuamini vipi?
 
Kwanza
1. Waziri aondoke (kwasababu ameshindwa kusimamia misingi imara ya kielimu, ilikukuza na kuimarisha Kiwango cha elimu Tanzania)
2. Waziri mkuu, ajirekebishe na arekebishe maamuzi yake ya kuwadharau waalimu pindi wanapo kuwa na shida, Kwani anajua matatizo yao na hataki kuyashughulikia. kwa kumsaidia tu!
a) Mshahara mdogo
b) Mazingira mabovu ya kuishi
c) Mazingira mabovu ya kufundishia
d) Madeni sugu yasiyo lipwa
e) Kuta sikilizwa pia
3. Wazazi pia wajaribu kubadilisha Design za maisha (kwani watoto wa siku hizi wamekuwa free sana, kufanya mambo ya kijinga tofauti na watoto wa kipindi cha nyuma)
4. Badilisha mitaala na Kurekebisha Baraza La mitihani
5. Kuboresha fursa za kujifunza kwa vitendo, Debates, Essays, na Mitihani ya kujishindanisha na kujiandaa pia!

natoa hoja
 
hili suala la kufeli halijaanza leo limeanza kujitokeza toka mwaka 2009 katika kipindi kama hicho hakuna jitihada zozote ambazo serikali ilizifanya kutatua tatizo hilo pia hivyo basi kwangu mimi naona kuwa tatizo ambalo limetokea hii leo kwa wadogo zetu hawa ni muendelezo wa matatizo ya kuanzia mwaka 2009 hivyo basi kwangu mimi nashauri tu kuwa hiyo tume itakayoundwa isitoe majibu ya tatizo la leo peke yake kwani itakuwa imesaidia sehemu ndogo sana ya tatizo
Ili tujilidhishe katika tatizo la elimu nchini hii tume iangalie zaidi ya hapo kwa maana ya kuwa ifanye uchunguzi yakinifu hata kama utachukua muda mrefu lakini mwisho wa siku ije na suluhisho la tatizo la elimu nchini
Pia viongozi wetu waache tabia ya kuongea kitu ambacho hakina uhakika mfano waziri wa elimu kipindi anatangaza matokeo alisema ya kuwa matokeo mabaya ya kidato cha nne yamesababishwa na ukosefu wa maabara kwa shule nyingi za serikali na pia uhaba wa walimu katika shule hizo
swali la kujiuliza ni je katika michepuo ya Arts ambako wanafunzi hawafanyi masomo ya sayansi matokeo ni mazuri? na pia katika shule za private ambako walimu wake hawategemei kijimshahara cha serikali napo kesi ndiyo hiyo
huyu ndiye waziri mwenye dhamana ya elimu tanzania anayejibu majibu mepesi kabisa katika suala la msingi kwa maoni yangu kwa harakaharak huyu waziri tume ije na mapendekezo ya kumuondoa katika nyadhifa hizo kwani kaongea jambo ambalo halijafanyiwa utafiti bado
 
Asante,me nashauri kua Wanafunzi wanaongia kidato cha kwanza wawe bora,maslahi ya walimu yaboreshwe,na wanafunzi wajitambue
 
Wanaotaka kunijua mimi ni Activist hapa Elimu ya Juu
 
Matokeo yamekua mabaya,yamezunguzwa mengi,toa maoni yako kama mdau tuweze kuwasaidia wanafunzi na Tulikomboe Taifa,maoni yote yatapelekwa Wizarani kuboresha.

wewe binafsi umechangia madogo kufeli... Umekimbia kituo chako cha kazi kitemitemi...sasa lile pengo uloiloliacha nani kaliziba!?, madogo wanafundishwa na nani sasa!!!?
 
Hebu tujaribu tuanzishe vyuo vingi vya ufundi kwa vitendo ambavyo udahili wake wa kujiunga ni kwa mtu yeyote aliyemaliza elimu ya shule ya msingi bila kujali anajua kusoma au hajui kusoma. Leo hii tumekusanya watoto wasiojua kusoma wala kuandika na kuwajaza kwenye shule za sekondari za kata, jamani sio watoto wote lazima kupata elimu ya sekondari. Matokeo yametoka tunaanza kulaumu walimu na serikali eti wameshindwa kusimamia elimu, hivi ni mwalimu gani wa sekondari ambae atakuwa tayari kuwafundisha watoto waliokaa miaka saba shule ya msingi na wakashindwa kuelewa kusoma na kuandika? wazazi tukae na watoto wetu tujitahidi kujua watoto wetu wanapenda kujifunza nini? Hebu tujaribu kujifunza kutoka kwa wenzetu, watoto wana vipawa mbalimbali kama michezo, sanaa, ufundi,udereva etc sasa sisi tumekusanya vipawa mbalimbali na kuwajaza kwenye shule za kata, tutegemee nini hapo form four?

Napendekaza, serikali ibadilishe baadhi ya shule za kata na kuwa vyuo vya ufundi kwa vitendo,
 
Matokeo yamekua mabaya,yamezunguzwa mengi,toa maoni yako kama mdau tuweze kuwasaidia wanafunzi na Tulikomboe Taifa,maoni yote yatapelekwa Wizarani kuboresha.
Kwakweli ni mjadala mpana.
Elimu ya sekondari haikuwa ya wote. Wenye sifa ya kuendelea na elimu ya sec ndiyo waendelee haya ni maigizo ya kupeleka watoto wote sec toka p7 na matokeo yake ndiyo hayo.
Walimu wathaminiwe kama watumishi wengine wa umma hatuwezi kuboresha kitu chochote ktk elimu bila kuanza na mwl. Mwl kama ana ari ya kazi watoto watasoma na kuelewa hata 'chini ya mti'.
Wazazi, walimu tushirikiane kuwalea watoto wetu ktk maadili mema. Mtoto aingiapo duniani anakuwa guided mpaka anapokuwa mtu mzima. Kama hawako tayari kujifunza hamna jinsi wanaweza fundishwa.
Tufanyie mitaala mapitio ili iende na wakati.
Selikari iwe makini.
Haiwezekani pesa ya selikari inafujwa hovyo na wafujaji hawachuliwi hatua yeyote alafu walimu wasiotimiziwa stahiki zao waendelee kufanya kazi kwa moyo.
 
cut off point ya kuindia kidato cha kwanza iwe ni mia moja. kwa kwale watakaofeli waende private school au waruhusiwe ku reseat kisheria maana mtu anaweza kufika la saba kwa mara ya kwanza asijui shuleni anatafuta nini lakini akiferi na kuonja uchungu wa kuferi anaweza kujianza upya baada ya kuruhusiwa kukariri la saba
 
Sijatoroka,nimeondoka,Kukaa Matipwili Bagamoyo4years inatosha
 
Hivi nani hajui kuwa:- posho za walimu na mshahara mzuri

1. watafundisha vizuri?
2. wanaodai hakuna maabara, hao hao lab teachers watabuni njia mbadala na watoto watapenda sayansi?
3. walimu waliokimbia ualimu wale wazuri watarejea ufungufu utapungua
4. huko vijijini wanasiasa wanakodai walimu hawataki watataka mshahara ukiwa bora
5. wanafunzi watabaki na walimu muda mrefu badala ya watoto kukaa na walimu muda mfupi na baadae wanaingia kwenye vishawishi na makundi na matendo mabaya
6. Heshima ya ualimu itaimarika na watafanyakazi yao inayowahusu badala ya kuwa wajasiriamali mtaani

Nwashangaa wanaodai elimu katelekezwa wakati wakigoma mnajifanya kulaani, watanzania ni mafirauni sana, mandumilakuwili, wanasura mbili moja mbele nyingine nyuma...madaktari hivyo siipendi nchi hii kwa umbumbumbu wetu, ukitetea serikali unajua unawapa kichwa?
 

[ Nasikia ametelekezwa na BABA YAKE ]
mkuu, unamjua huyo BABA aliyekusudiwa hapa?
 
Hawa watoto 63%+ wapewe nafasi ya mwisho ya kufanya tena mtihani na serikali ikubali kubeba gharama. Kwa nchi hii si gharama kubwa sana ni kiasi cha kuacha kununua Shangingi V8 moja tu. Tusiwadharau hawa jamaa kwani wapo wengi wanaweza kuonyesha maajabu katika marudio pia wakiachwa bila msaada wowote wapo watakaoshawishika kuingia kwenye uhalifu na kesho ukasikia waziri au kiongozi fulani "kaenda" kwani hawa wako tayari kwa lolote wakishafikia hapa.
 
Matokeo yamekua
mabaya,yamezunguzwa mengi,toa maoni yako kama mdau tuweze kuwasaidia
wanafunzi na Tulikomboe Taifa,maoni yote yatapelekwa Wizarani
kuboresha.

Tume iliyoundwa itatoa maoni,au na wewe unamiliki Tume yko.
 
UONGOZI NI SAWA NA UDEREVA UNAPOENDESHA BASI LA ABIRIA HAINA MAANA WE NDIO UNAJUA KULIKO WOTE ULIOWAPAKIA KATIKA BASI LAKO. BALI KWAKUWA USKANI NI MMOJA NDO MAANA WEWE UMEPEWA DHAMANA YA KULIONGOZA BASI HILO, HIVYO FIKRA ZA SERIKALI YETU TUKUFU YA CCM INAVYODHANI ATI KIONGOZI NDIYE ANAJUA KULIKO WANANCHI ANAOWAONGOZA. NDOMAANA KUNAKAULI MBALIMBALI ZILIWAHI KUTOLEWA KUMDHALILISHA MWALIMU KA VILE KIONGOZI MMOJA WA SERIKALI ALIWAHI KUSEMA (1)mwalimu akiona mshahara mdogo basi atafute kazi yenye mshahara mkubwa, (2)walimu ni wengi hivyo hatuwezi kuwalipa mishahara mizuri, (3)mgomo wa walimu hauna madhara kama ule wa madaktari, HIZI NI BAADHI YA KAULI ZA KEJELI NA WALIMU WANAZIONA NA ZINAWAKELA MNO.
KUNA WILAYA MOJA HUKO MKOA WA MTWARA WALIMU WAKE ASIOPUNGUA 18 WALIKATIWA MSHAHARA KIMAKOSA KWA ZAIDI YA MIEZI MIWILI LAKINI HAKUNA ALIYEJALI KUWARUDISHIA MSHARA WAO KWA WAKATI MATOKEO YAKE WAKATI WALIMU HAW WAKIANGAIKA KUJIKIMU MKURUGENZI HAKUWAPA HATA SHILINGI YA KUWAWEZESHA WAO KUISHI KATIKA KIPINDI HICHO BALI TULISHUHUDIA MKURUGENZI AKIPANGA SAFARI NA WAHESHIMIWA MADIWANI WAKE KUTEMBELEA MIKOA KADHAA NA KUWALIPA POSHO WOTE KWASIKU ZOTE WALIZO TUMIA KUTALII HUKO, MATOKEO YAKE WALIMU HAWAJALIPWA MISHARA HIYO WANAYOIDAI WAKIULIZA WANADAI WAMETUMA MAJINA YAO HIVYO SERIKALI ITAANGALIA KAMA ITAWEZA KULIPA AU LA, SASA NI MWAKA UMEKATIKA TANGU TUANZE KUDAI, JE WE MTANZANIA UNGEKUWA MWALIMU HUYU UNGEFANYA KAZI KWA MOYO? NI WAKATI WA MABADILIKO VIONGOZI WAZEMBE WATOKE WAJE WAWAJIBIKAJI.
 
6. in addition, mafunzo ya waalimu yatolewe kukidhi mahitaji ya utoaji wa elimu yaani mtaala7. wanafunzi wapewe mafunzo kwa vitendo kama ilivyo ktk shule binafsi, vyuo vya kilimo na ufundi8. kabla ya mitihani wanafunzi waandaliwe kitaaluma na kisaikolojia kukabili mitihani ipasavyo9. somo la kiingereza lipewe kipaumbele ktk mafunzo kama njia ya mawasiliano ya kukabili matakwa ya kitaaluma10. mtindo wa kuwaingiza kwa mkururowatoto wenye alama chini ya 50 kama ilivyokuwa hapo zamani11. watoto wawe subjected to IQ Test ili kupata wale wanaostahili kukabili masomo ya secondary, watakaofeli wapewe mafunzo ya ujasiriamali kwani watakaoishia dar. vii wao sio wa kwanza kwani waliopo wanaendesha maisha vizuri kuliko maprofesa12. uwekwe mkazo wa kusimamia taaluma toka dar. la i-vii then form i-form iv
 
6. in addition, mafunzo ya waalimu yatolewe kukidhi mahitaji ya utoaji wa elimu yaani mtaala 7. wanafunzi wapewe mafunzo kwa vitendo kama ilivyo ktk shule binafsi, vyuo vya kilimo na ufundi 8. kabla ya mitihani wanafunzi waandaliwe kitaaluma na kisaikolojia kukabili mitihani ipasavyo 9. somo la kiingereza lipewe kipaumbele ktk mafunzo kama njia ya mawasiliano ya kukabili matakwa ya kitaaluma 10. mtindo wa kuwaingiza kwa mkururo watoto wenye alama chini ya 50 uachwe ili matokeo yawe kama ilivyokuwa hapo zamani 11. watoto wawe subjected to IQ Test ili kupata wale wanaostahili kukabili masomo ya secondary, watakaofeli wapewe mafunzo ya ujasiriamali kwani watakaoishia dar. vii wao sio wa kwanza kwani waliopo wanaendesha maisha vizuri kuliko maprofesa12. uwekwe mkazo wa kusimamia taaluma toka dar. la i-vii then form i-form iv 13. watoto wajenge tabia ya kjisomea vitabu na kufanya mazoezi ya ziada baada ya ratiba ya masomo wakti wa likizo na muda wa nje ya masomo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…