Hollywood ni wakali kwa almost mambo mengi kama sio yote yanayohusu Movie!
Kinachonifanya niwape tano hollywood zaidi ni uwezo wao kutengeneza kisa cha mazingira ya sehemu yoyote duniani na kukidhi utamaduni wa watu husika.
Mnaozungumzia mapenzi, tujikumbushe "mississipi massala" ya Denzel Washngton, ok hii kitambo tujikumbushe "slumdog millionaire".
Hollywood wanaweza kutoa muvie ya kisa cha sehemu yoyote, mfano "The last king of scotland" (uganda), "Hotel Rwanda", "Tears of the Sun" (nigeria), "The kingdom" (iraq) "Black hawk down" (Somalia), "The Man on fire" (mexico)!
Na zingine kibao tu wanajamvi tukumbushane.
Kwa hili nimekuwa nawakubali sana Hollywood, afu pia jingine ni kwamba kwenye movie zao nyingi ile dhana ya kuigiza inaondoka utafikiri kweli hapa namaanisha hasa kwenye stunt, matukio kama majeraha, na matukio makubwa mfano movie ya "2012" unaweza ukadhani dunia nzima ilikuwa inahusika, pia tujikumbushe Titanic, pia uwezo wao wa kutengeneza matukio ya ndani sana ya nchi yao hasa serikalini mfano "24hrs series", au "prison break" (zipo nyingi sana za hivyo, tukumbushane zaidi).
Hapo hatujazungumzia za mambo ya kisayansi na tchnology, sikuhizi kuna animation.... movie kama AVATAR, hii ilikuwa kali sana na story japo kwa kuzitaja ni chache sana.
Bollywood ni wapo vizuri sana, na ni wakongwe sana ila kukumbatia sana "UHINDI" kuliwaondoa kwa kiasi flani kwenye soko la mataifa yasiyoongea kihindi.
Ila bado ni wajanja coz waliliona na wamefanya mapinduzi makubwa sana kwenye game yao, Movie zao za kuanzia miaka ya 2000 wamebadilika sana afu nyingi wana-act ulaya na America.
Jana nilikuwa naangalia "MY NAME IS KHAN" ameigiza Shuh Rukh Khan, kweli nikakuali mabadiliko ya msingi wamefanya na ni bonge la movie, hamna mambo ya kuimbaimba(vikota), humo wameichezea marekani hadi wamemuweka "Obama"...... poa tutaijadili next time kama maada itarusu.
Mwisho wa siku HOLLYWOOD ni WAKALI sana sana kuliko industry zote duniani.