Bom!bom!bom! Uhasi arusha.

R-CHUGA

Member
Joined
Mar 23, 2012
Posts
77
Reaction score
8
Mabomu ya machozi yanaendelea kurindima ndani ya chuo cha uhasibu yapata saa moja sasa baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha kususa kuzungumza na wanafunzi ambao mwenzao ameuawa kwa kuchomwa kisu.Mkuu huyo amekataa kuongea na wanafunzi kwa kusema kwamba hawana nidhamu ndipo wanafunzi walipoamua kurusha chupa kwenye gari lake.
 
Yes! Ndiyo tabu ya uongozi mbovu wa serikali legelege ya jakaya!

Na nimepata kuambiwa ni kwamba huyo mwanafunzi ameuawa jana jioni majira yapata saa tatu usiku.

Update................zitafuata!
 
Sasa wewe kitu gani kinakufahisha hapo? kurusha machupa? Aisee, this is very serious.


Viongozi wanapaswa kujifunza jinsi ya kuishi kulingana na mazingira, sio kila eneo linahitaji kutumia nguvu na Userikali, wakati mwingine Kiongozi anapaswa kuwa Mpole na Mnyenyekevu kwa wananchi wake ili mradi adumishe amani. Sasa kuna haja gani ya kuwaambia wanafunzi kuwa hawana nidhamu wakati wa msiba. Kwa nini asisubiri msiba upite aende kuongea nao kama Mzazi.
 
Poleni sana kwa msiba na mabomu juu yake.Hii kali! Wafiwa wanapigwa mabomu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…