Bomba la gesi toka Mtwara ulinzi mkali wa Camera

Bukya

Senior Member
Joined
Apr 1, 2014
Posts
195
Reaction score
121
Bomba la gesi litokalo Mtwara limewekewa ulinzi mkali unaotumia camera za CCTV. Kila baada ya km 50 kuna security cabin na watu wanaofanya kazi kwa saa 24.
 
Tuwaulize watawala wanaogopa nini? Wanajua kuwa watu wa Mtwara hawajaridhika na kinachoendelea. Wanaogopa risasi tu za polisi. Kuna siku wataziona kama maji!
 
Hapo kuna kampuni za wakubwa zimeshapewa tender za kufunga cctv na kampuni ya ulinzi!! Sasa kaangalie gharama zake ndo utalia! Ni zaidi ya gharama ya kuhudumia kikosi cha jeshi lugalo!!

Kweli kabisa!
Inatia uchungu sana
 
Sitajadili historia ya hilo bomba na madhila yalowakuta wa Mtwara ila ni muhimu sana kulinda miundombinu yetu iliyogharimu akili, muda, jasho, maisha na pesa zetu.

Ifanyike hivyo kwenye njia za umeme, reli, madaraja yote na barabara kuu pia zile za BRT.

Kuhusu aina ya ulinzi, kwa njia za umeme na reli, wanaweza kutumia vijana wa vijiji njia zinakopita wawe sungusungu. Hili pia litapanua wigo wa ajira vijijini. Ndivyo Tanroads na Tanesco wanafanyaga kufyeka maeneo yao.

CCTV pia ziwepo kwenye maeneo korofi au tata mfn. Mbuga za wanyama.

Tulinde vilivyotugharimu. Kwa wenzetu huko mbele kuna miundombinu ina karne zaidi ya moja. Ulinzi wake ni balaa tupu.
 
Tuwaulize watawala wanaogopa nini? Wanajua kuwa watu wa Mtwara hawajaridhika na kinachoendelea. Wanaogopa risasi tu za polisi. Kuna siku wataziona kama maji!
Ndugu uliza uambiwe maana. Mabomba ya gesi na mafuta duniani pote yanalindwa tena kwa nchi zilizo makini wanatumia Teknolojia ya hali ya juu kama SCADA! Hiyo ni Vital Installations.
 
Mabomba ya mafuta ndio ya maana kuliko installations zingine Tanzania, mbona hazina ulinzi mkali wa namna hiyo! Mbona TAZAM haina huo ulinzi mpaka leo? Naomba jibu
 
sio bamba bomba siku nyingine jifunze kiandika
 
Mabomba ya mafuta ndio ya maana kuliko installations zingine Tanzania, mbona hazina ulinzi mkali wa namna hiyo! Mbona TAZAM haina huo ulinzi mpaka leo? Naomba jibu
Unatafuta ligi ya majibizano. Kwa msaada hebu google upate majibu au waulize watalaamu wa sekta ya mafuta na gesi (TPDC) wakupe majibu maana naona huitaji kuelewa.
 
Nauliza mbona TAZAMA haina ulinzi? I do not need to google this !
 
Back
Top Bottom